East Afrika Derby Uganda kukabana koo na Rwanda CHAN
Miamba wa Afrika Mashariki Amavubi ya Rwanda na Uganda Cranes watamenyana jumatatu usiku katika mchuano wa pili wa kundi C kuwania kombe la CHAN uwanjani Reunification mjini Doula.
Kocha wa Rwanda Johnny McKinstry aliyeiongoza Rwanda kucheza hadi robo fainali mwaka 2016 wakiwa nyumbani ataiongoza Uganda Cranes katika mechi ya Jumatatu dhidi ya msaidizi wake mwaka 2016 Vincent Mashami ambaye ndiye kocha mkuu wa Rwanda katika makala ya mwaka huu.
Rwanda itamtegemea sana mshambulizi Jaques Tuyisenge wa APR huku Uganda ikitegemea huduma za mshambulizi wa KCCA Brian Aheebwa.
Waganda pia wamekuwa na matayarisho mazuri baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano yaliyotangulia fainali hizo za CHAN mapema mwezi huu nchini Cameroon kwa kushinda mechi mbili dhidi ya Zambia na Niger na kutoka sare na wenyeji Cameroon.
Uganda inashiriki CHA N kwa mara ya 5 huku Rwanda wakipiga kwa mara ya pili.
Kundi hilo pia linajumuisha mabingwa watetezi Moroko na Togo wanaoshiriki kwa mara ya kwanza.
Mechi zote mbili zitarushwa mbashara na runinga ya taifa KBC Channel 1.
Moroko dhidi ya Togo saa moja usiku na Uganda dhidi ya Rwanda 10pm