DRC, wanamgambo wa Kiislamu wawauwa watu 20

Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu walishambulia vijiji viwili mashariki ya Congo na kuwauwa watu 20.

Hii ni sehemu ya msururu wa mauaji yanayoendelea nchini humo ambayo Umoja wa Mataifa unasema huenda yakachukuliwa kuwa mauaji ya halaiki.

Kundi lililojihami kutoka Uganda kwa jina Allied Democratic Forces limekuwa likiendeleza shughuli zake mashariki ya Congo kwa zaidi ya miongo mitatu ambapo limewaua raia zaidi ya elfu moja tangu mwaka jana.

Umoja wa Mataifa unasema kwamba ghasia zinazosababishwa na kundi hilo zimeongezeka mwaka huu kufuatia juhudi za wanajeshi za kuliangamiza.

Kundi hilo sasa limeondoka kwenye kambi walimokuwa wakikaa na kubuni makundi madogo madogo yanayoendeleza vurugu. Kwa mujibu wa umoja wa mataifa watu zaidi ya nusu milioni wametoroka makwao kutokana na vitendo vya kundi hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *