Dominic Thiem atwaa ubingwa wa Us open

Dominic Thiem wa Austria  alihitaji maarifa ya ziada, kabla ya kumlemea Alexander Zverev wa Ujerumani na kushinda  taji ya Us Open kwenye fainali ya wanaume mapema leo mjini Newyork.

Fainali hiyo ilihitaji seti 5 ili kubaini bingwa, ambapo  Thiem alipoteza seti za kwanza mbili  2-6, na 4-6,kabla ya kujizatiti na kushinda seti tatu zilizofuatia 6-4,6-3 na 7-6.

Thiem aliye na miaka 27, ndiye mchezaji wa kwanza kutwaa ubingwa wa taji ya Us Open baada ya kupoteza seti mbili za ufunguzi na ndiye mchezaji wa kwanza kutoka Austria kunyakua taji ya Us Open .

Pia Thiem ndiye mchezaji wa pili kutoka Austria kushinda taji ya Grand Slam baada ya Thomas Muster kunyakua ubingwa wa Roland Garros mwaka 1995.

“ilikuwa fainali ngumu ,lakini nafurahia ushindi wangu “akasema Thiem baada ya fainali.

Ushindi huo wa Thiem unampa taji ya Us open na shilingi milioni 322 za Kenya au dola  milioni 3 za Marekani.

Naomi Osaka alinyakua taji ya wanawake mapema jana alipommshinda Victoria Azarenka kutoka Belarus kwenye fainali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *