Brian Mandela ajiunga na Mamelodi Sundowns kwa mkataba wa miaka mitatu
Difenda wa Kenya Brian Onyango Mandela amesaini mkataba wa miaka mitatu kuwachezea mabingwa wa Afrika Kusini Mamelodi Sundowns.
Mandela amejiunga na Mamelodi maarufu kama the Brazillians akitokea Maritzburg United kwa uhamisho usio wa malipo .
Awali beki huyo aliichezea timu ya Santos mwaka 2012 alipowasili Afrika kusini kwa mara ya kwanza kabla ya kujiunga na SuperSport United.
Mandela aliye na umri wa miaka 26 anafuata nyaoyo za kapteini wa zamani wa Harambee Stars Musa Otieno aliyeichezea timu ya Santos baina ya mwaka 1997 na 2011.
Beki huyo alikuwa amesainiwa na timu iliyopandishwa ngazi maajuzi katika ligi kuu ya Afrika Kusini Tshakhuma Tsha Madzivhandila lakini hakuwa amesaini kandarasi nao .
Akiwa Mamelodi ,Mandela atacheza pamoja na kipa wa kilabu hiyo ya Mamelodi Denis Masinde Onyango ,ambaye na nahodha wa Uganda Cranes.
Onyago aliinza soka humu nchini kenya akiichezea timu ya Posta Rangers mwaka 2010 ,kabla ya kujiunga na Tusker Fc kati ya mwaka 2011-2012 na kisha akajiunga na Santos ya Afrika kusini baina ya mwaka 2012-2105 akicheza mechi 48 na kufunga mabao matatu kabla ya kuhamia Maritzburg United kutoka mwaka 2015 hadi 2019 aliposakata michuano 77 na kufunga mabao 8.
Upande wa timu ya taifa Harambee Stars Mandela amecheza mechi 22 na kufunga mabao 2 na akiwa Afrika kusini atakutana na Mkenya mwingine kiungo Anthony Akumu wa Kaizer Chiefs.
Mamelodi imenyakua taji ya ligi kuu Afrika kusini mara 10 ,ya mwisho ikiwa mwaka jana huku pia wakijivunia kunyakua kombe la ligi ya mabingwa Afrika mara moja.