Diego Maradona aaga dunia akiwa na umri wa miaka 60
Nguli wa soka Diego Armando kutoka Argentina amefariki dunia Jumatano jioni kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 60.
Maradona ameaga dunia akiwa nyumbani kwake kwa mjibu wa wakili wake ikiwa wiki mbili tangu aondoke hospitalini alikofanyiwa upasuaji wa ubongo .
Maradona anatambulika kama mmoja wa wanasoka maarufu na shupavu wa karne hii alipoisaidia Argentina kunyakua kombe la dunia mwaka 1986 akiwa nahodha .
Pia marehemu anakumbukwa kwa kufunga bao kwa mkono bao lililoibandua Uingereza katika robo fainali ya kombe la dunia mwaka 1986 na kuliita bao hilo ‘Hand of God’ .

Anakumbukwa pia kwa kutimuliwa kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 1994 kwa kupatika kuwa mtumizi wa dawa zilizoharamishwa zinazopatika katika dawa ya kulevya ya Cocaine.
Masaibu yake yalianza kuongezeka baada ya kusataafu kutoka soka iliporitowa kuwa alikuwa mraibu wa dawa za kulenya haswa Cocaine na pia mlevi wa starehe zilizochangia matatizo ya yake mengi ya kiafya ikiwemo tatizo la mshtuko wa moyo .

Katika enzi zake za usakati kambumbu Maradona alinyakua taji ya ligi kuu Italia Serie A akiwa na kilabu cha Napoli miaka ya 1987 na 1990, kombe la Italia mwaka 1987 na lile la Uefa Cup mwaka 1991.
Hadi kifo chake Maradona amekuwa mkufunzi wa kilabu cha Argentina Gymnasia Esgrima na alikuwa tayari amefanyiwa upasuaji mara mbili.
MOLA AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA