Diamond alaumiwa kwa kuiga!

Mwanamuziki nyota wa Tanzania Diamond amejipata lawamani kwa zamu nyingine baada ya kile kinachosemekana kuwa anaiga mawazo ya wasanii wengine katika kuunda video za muziki wake.

Kwenye Video ya wimbo kwa jina “litawachoma” ambao umeimbwa na Zuchu akimshirikisha Diamond, kuna sehemu Diamond anaimba akiwa ameketi na wengine na nywele zake zinasukwa kwa kutumia lulu ndogo ndogo na kuna picha ambayo ilikuwa tayari imetokea yake Nandy akiwa amesonga hizo lulu kichwani.

Nandy kwenye akaunti yake ya Instagram aliweka picha ya Diamond kwenye wimbo huo na ile yake ya awali na maneno “God is Good”. Kwenye comments mashabiki walionekana kumkanya asijaribu kuanzisha malumbano na Diamond.

Wazo la video ya “Litawachoma” linasemekana pia kuwa la wimbo wa mwanamuziki “Tobe Nwigwe” wa Houston Marekani ila ana asili ya Nigeria.

 

Mchekeshaji wa marekani kwa jina “Kevon” ndiye alianzisha minong’ono mitandaondi na video yake akidai kwamba Diamond na Zuchu wameiba wazo la rafiki yake Tobe Nwigwe.

Kevon anasema alipata pendekezo la you tube kwamba atizame video ya Diamond na Zuchu ndio akapata inafanana na ya rafiki yake.

Aliachia video akiwa amekasirika na kumkashifu mwelekezi wa Zuchu na Diamond kwa kuchukua wazo hilo la rafiki yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *