Diamond akutana na shabiki sugu

Mwanamuziki wa Bongo Diamond Platinumz nusura adondokwe na machozi pale alipokutana na shabiki wake sugu.

Alikuwa amemaliza kazi ya kutumbuiza kwenye uwanja wa Tanganyika Packers ambapo chama kinachotawala nchini Tanzania cha CCM kilikuwa kimeandaa mkutano wa kujjipigia debe.

Jamaa huyo anampenda Diamond sana kiasi cha kuchora sura ya Diamond Platinumz na Nembo ya Wasafi kwenye kifua na shingo lake.

Diamond mwenyewe alimsaidia shabiki huyo kupanda kwenye gari lake na alipoona michoro hiyo kwa karibu akamkumbatia na kupandwa na hisia.

 

 

Shabiki huyo kwa jina Majaliwa Juma alifichua pia kwamba alibadili dini toka Ukristo hadi uisilamu kwa ajili ya mapenzi yake kwa Diamond.

Wawili hao waliandamana hadi nyumbani kwa Diamond kwa mazungumzo zaidi. Na kama njia ya kushukuru kwa mapenzi hayo ya dhati, Diamond alimpa bwana huyo mdogo hela milioni moja za Tanzania aanzishe biashara.

 

Zaidi ya hapo alimpa ahadi ya kumtangazia biashara hiyo bila malipo kwenye vituo vya Wasafi Media hadi biashara yenyewe ikue.

Diamond pia atatangaza biashara hiyo inayotarajiwa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo ana wafuasi wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *