DCI yachunguza walaghai wa mitandaoni wanaowahadaa wanafunzi wa kike

Idara ya upelelezi wa jinai imeanzisha uchunguzi kuhusu kundi la walaghai wa mitandaoni wanaowahadaa wanafunzi wa kike wa shule kuondoka nyumbani mwao kuhudhuria karamu zinazoendelea kwa siku kadhaa.

Walaghai hao wanatumia nambari za simu za kimataifa hata ingawa wanaendeleza shughuli zao jijini Nairobi.

Idara hiyo inawashauri wazazi kuchunguza mienendo ya watoto wao na shughuli zao mitandaoni.

Hayo yamewadia siku moja baada ya idara hiyo kubainisha kwamba wasichana sita walishawishiwa kutoroka nyumbani kwao kupitia ukurasa wa instagram hadi siku ya Ijumaa wakati maafisa wa polisi walipogundua mahali walikokuwa.

Wasichana hao walitoweka Jumamosi iliyopita huku jamaa wao mmoja akisema walaghai hao waliwasiliana nao kupitia nambari ya simu iliyosajiliwa Marekani.

Baadhi ya wazazi kutoka mitaa ya Komarock na Kayole wameripoti kutoweka kwa watoto wao wa kike kwa siku kadhaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *