Curtis Olago kuifunza Chipu kwa miaka miwili

Curtis Olago ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya raga kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 maarufu kama Chipu kwa mkataba wa miala miwili.

Mtihani wa kwanza kwa Olago utakuwa kuiongoza Chipu kutetea kombe  la  Barthes .

Kiungo huyo wa zamani wa timu ya taifa na klabu ya Mean Machine kaunti ya  Kisumu pia amewahizichezea timu za  Impala, Nondescripts na KCB kabla ya kuanza ukufunzi ambapo aliiwezesha KCB kutwaa ubingwa wa ligi kuu mara 4 mwaka 2015,2017,2018 na 2019.

Kenya wataanza kutetea kombe hilo la Barthes katika kundi A dhidi ya Madagascar,Tunisia na Zambia huku kundi B likiwa na Senegal,Namibia,Zimbabwe na Cote d’ Ivore.

Pool A:
Kenya
Madagascar
Tunisia
Zambia

Pool B:
Namibia
Senegal
Zimbabwe
Côte d’Ivoire

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *