Comoros yaitoa Kenya Pumzi Kasarani

Harambee Stars chini ya kocha mpya Jacob Ghost Mulee imelazimika kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Comoros katika pambano la kundi G kufuzu kwa kombe la AFCON mwaka ujao .

Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani Jumatano usiku.

Kiungo Yousef M’changa aliwaweka wageni Comoros Uongozini kwa tobe la mkwaju wa adhabu kunako dakika ya 26 kabla ya kulishwa kadi ya pili ya njano katika dakiak ya 41 na kuondolewa uwanjani ,akiwalazimu wenzake kucheza zaidi ya dakika  50 .

Kipindi cha pili kocha wa Harambee Stars alimwondoa uwanjani Samwel Olwande na kumjumuisha David Owino katika safu ya ulinzi  na baadae Stars wakaanza kushmabulia mlango wa wageni yaliyozaa matunda huku Masud Juma anayecheza soka ya kulipwa nchini Algeria akiwaepushia wakenya fedheha kwa bao la kusawazisha katika dakika ya 65.

Kenya watajilaumu kwa kukosa kutumia upungufu wa wachezaji wa Comoros huku kipa wa wageni  Ali Ahamada akipangua mikjwaju na amshambulizi yote ya wenyeji.

Comoros watawaalika Kenya Novemba 15 kwa pambano la marudio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *