City Stars waizidia maarifa Bandari Fc ligi kuu FKF
Mabingwa wa ligi ya NSL Nairobi City Stars wamerejelea tambo za ushindi baada ya kustahimili wakati mgumu kabla ya kuibwaga Bandari fc mwabao 2-0 katika mchuano wa ligi kuu Fkf uliopigwa Ijumaa alasiri katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.
Baada ya kipindi cha kwanza kuishia sare tasa , wenyeji City stars waliimarisha mchezo kunako kipindi cha pili huku mshambulizi Anthony Kimani akipachika bao la kwanza dakika ya 60 na baadae Bernard Odhiambo wa Bandari akajifunga na kuwapa City Stars bao la pili katika dakika ya 67 huku mechi ikudumu kwa matokeo hayo hadi kipenga cha mwisho.
Mechi nne za ligi kupigwa Jumamosi Western Stima wakiikabili Tusker Fc uwanjani Moi Kisumu nao Afc Leopards watakuwa nyumbani kupimana nguvu dhidi ya Sofapaka huku Kariobangi Sharks wakiwa na miadi dhidi ya Bidco united mech zote zikichezwa saa tisa na kisha mabingwa watetezi Gor Mahia wachuane na wanajeshi Ulinzi Stars saa kumi alasiri katika uwanja wa taifa wa Nyayo.
Jumapili Kakamega Homeboyz watamenyana na KCB ugani Kasarani,Vihiga United wakabane koo ya Nzoia Sugar kiwarani Mumias Sports Complex huku Posta rangers wakifunga ratiba nyumbani Utalii Grounds kuanzia saa tisa unusu.
Hata hivyo timu za Zoo Fc na Mathare United hazitacheza wikendi hii baada ya kupigwa marufuku na FKF kwa kukaidi kusaini mkataba baina ya FKF na Star Times.