Chipukizi wa Kenya chini ya umri wa miaka 17 kuingia kambini Jumanne kujiandaa kwa CECAFA

Timu ya taifa ya Kenya kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17  inatarajiwa kuripoti kambini Jumanne kujiandaa kwa mashindano ya Cecafa yatakayoandaliwa mjini Kigali Rwanda mwezi ujao.

Shirikisho la kandanda nchini lilikamilisha zoezi la uteuzi wa vijana hao mwishoni mwa juma lililopita baada ya kuzuru mikoa yote minane kutambua wachezaji walio na talanta ili wajumuishwe kwenye timu hiyo.

Zoezi la uteuzi liliongozwa na kocha mkuu wa timu ya taifa kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 17  Oliver Page na lilianza rasmi  Novemba 13 kwa maeneo ya  Nairobi na  Thika huku  Nakuru, Kisumu, Magharibi , Machakos, Pwani, na  Meru wakifanya pia zoezi hilo .

Uteuzi wa wachezaji mkoani pwani

Kenya imejumuishwa kundi B katika mashindano yaCECAFA yakatoandaliwa Rwanda kati ya Disemba 13 na 28 mwaka huu pamoja na  Uganda na  Ethiopia  ambapo timu mbili bora kutoka mashindano hayp zitafuzu kucheza mashindano ya AFCON nchini  Morocco  Julai mwaka ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *