Chepkoech na Birgen watamba Ujerumani

Wakenya  Bethwell Birgen na  Beatrice Chepkoech  walitwaa ushindi katika mbio za mita 3000 kwenye mashindano ya ukumbini  maarufu kama World Athletics Indoor Tour Gold meeting yaliyoandaliwa Ijumaa usiku mjini Karlsrue Ujerumani.

Birgen alichomoka na kuwaacha wenzake katika umbali wa mia 2000 baada ya kusaidiwa na wapiga kasi huku akikata utepe kwa dakika 7 sekunde 34 nukta 12, na kuingia kwenye madaftari ya kumbukumbu kuwa mwanariadha bora wa Kenya katika mashindano ya ukumbini.

Mohammed Katir wa Uhispania na Jimmy Grassier kutoka Ufaransa walinyakua nafasi za pili na tatu mtawalia.

Kwa upande wake mshikilizi wa rekodi ya dunia na bingwa wa dunia katika mita 3000 kuruka viunzi na maji Beatrice Chepkoech aliibuka mshindi kwa dakika 8 sekunde 41 nukta 98  , akifuatwa na Worku kwa dakika 8 sekunde 42 nukta 22 naye Courtney akatwaa nafasi ya tatu  kwa dakika 8 sekunde 42 nukta 41 .

Beatrice Chepkoech wins the 3000m at the World Athletics Indoor Tour meeting in Karlsruhe (Gladys Chai von der Laage)
Beatrice Chepkoech akishinda mbio za  3000  picha (Gladys Chai von der Laage) 

Shindano hilo lilikuwa la kwanza la ukumbini mwaka huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *