Chelsea na PSG zafuzu nusu fainali ya ligi ya mabingwa ulaya licha ya kushindwa

Paris St Germain ya Ufaransa  na Chelsea ya Uingereza zimetinga nusu fainali ya kombe la ligi ya mabingwa barani ulaya licha ya kupoteza mechi za marudio  za robo fainali Jumanne usiku.

Mabingwa wa Ufaransa PSG kwa walilipiza kisasi cha kushindwa na Bayern Munich kwenye fainali ya mwaka jana ,na kuwatimua katika kwota  fainali kwa magoli ya ugenini ,baada ya mechi kumalizikia sare ya 3-3.

Munich walipata ushindi wa bao 1-0 ugenini Parc De Princess Jumanne usiku  kupitia wa Maxim Chuopo Moting lakini  matumaini ya kupata bao la pili ambalo lingewafuzisha yakazamishwa huku wenyeji wakisaidiwa na ushindi wa magoli 3-2 katika mkumbo wa kwanza ugani Allienz Arena.

Psg watakuwa wakipiga nusu fainali ya kombe hilo la kifahari kwa mara ya pili mtawalia ,baada ya kucheza hatua hiyo msimu uliopita.

Psg watakutana kwenye semi fainali na mshindi wa kwota fainali  kati ya Manchester City na Borusia Dortmund.

Katika marudio ya kwota fainali iliyosakatwa mjini Seville Uhispani,Chelsea waliokuwa wameishinda FC Porto ya Ureno magoli 2-0 katika mkumbo wa kwanza magoli waliangushwa bao 1-0 .

Porto walipata bao hilo la ushindi dakika ya nne ya ziada katika kipindi cha pili kupitia kwa  Mehdi Taremi,huku  Chelsea wakifuzu kupiga nusu fainali ya kombe hilo kwa mara  ya  8 ikiwa timu pekee ya Uingereza kufuzu kwa hatua hiyo mara nyingi zaidi  , pia ikiwa semi fainali ya kwanza kwa vijana wa Thomas Tuchel tangu mwaka 2014.

The Blues watachuana katika nusu fainali  baina ya mwisho wa mwezi huu na mwanzoni mwa mwezi ujao  na mshindi wa robo fainali ya Jumatato baina ya Liverpool na Real Madrid,Los Blancos wakizuru Anfield wakijivunia uongozi wa 3-1.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *