Charles Mneria awika katika mbio za kukata mbuga za Magereza

Charles Mneria wa makao makuu ya magereza ndiye bingwa  mbio za nyika za magereza za kilomita 10 zilizoandaliwa Jumamosi katika uwanja wa chuo cha mafunzo ya makurutu KPTC mjini Ruiru.

Mneria aliye na umri wa miaka 24 aliongoza kutoka mwanzo hadi mwisho na kukata utepe kwa dakika 30 sekunde 15 huu ukiwa ushindi wake wa tatu mtawalia katika mbio za nyika msimu huu baada ya kusinda misururu ya kitaifa .

Mneria amesema alikuwa kiyatumia mashindano ya Jumamos kujiandaa kwa majaribio ya kitaifa ambako atawania tiketi ya kushiriki mita 10000 kwenye micehzo ya Olimpiki baina ya Julai na Agosti mwaka huu.

“Target yangu kubwa mwaka huu ni kwenda Olympics mita 10000″akasema Mneria

Boazb Kiprugut kutoka mkoa wa kati aliibuka wa pili kwa dakika 30 sekunde 42 nukta  63 naye Wilfred Kimitei kutoka pwani akamaliza katika nafasi ya tatu .

Wanariadha bora watakaochaguliwa wataiwakilisha idara ya magereza kwenye mashindano ya kitaifa ya mbio za nyika  tarehe 13 mwezi ujao  huko Kisii Golf Club ambapo chama cha riadha Kenya kitateua timu itakayoshiriki mashindano ya Afrika ya mbio za Nyika mjini Lome Togo kati ya tarehe 6-7  mwezi Machi mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *