Charger aongoza timu ya Kabras kunyakua nafasi 3 za kwanza baada ya miaka 10 katika mashindano ya Soysambu KCB Rally

Baldev Charger aliibuka mshindi wa mkondo wa kwanza wa mashidnano ya kitaifa ya mbio za magari mwishoni mwa Juma lililopita huko Soysambu ambapo madereva walipata fursa ya kujaribu mkondo utakaotumiwa wakati mashindano ya dunia WRC baadae mwaka huu.

Charger aliongoz timu yake ya magari ya timu ya Kabras kutwaa nafasi tatu za kwanza ,ambapo Tejvir Rai na Onkar Rai walinyakua nafasi za pili katika usanjari huo.
“Imekua fahari kuu kushinda nafasi tatu za kwanza kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10,tulianza kujipanga mwaka jana kwa mashindano ya majaribio na tulijua yale tungekumbana nayo katika mkondo wa mashindano hayo”akasema Charger

Mashindano hayo yataelekea kaunti za Nairobi na Nakuru kati ya tarehe 24 na 27 mwezi huu.

Charger anaongoza msimamo wa kitaifa KNRC kwa pointi 33 ,akifuatwa na Tejveer Rai kwa alama 25 huku Onkar Rai akiwa wa tatu kwa pointi 23 baada ya mkondo wa kwanza.

Ian Duncan ni wa 4 kwa alama 19 huku Eric Bengi akifgunga tano bora kwa pointi 17.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *