Chanjo ya China dhidi ya COVID-19 yaonyesha ufanisi

Watafiti wanasema majaribio ya chanjo dhidi ya COVID-19 iliyotayarishiwa nchini Uchina yameonesha ufanisi.

Majaribio ya chanjo kadhaa yanaendelea nchini humo na baadhi ya chanjo hizo zimeanza kutolewa kwa binadamu.

Kwa mujibu wa wataalam, Chanjo ya Sinovac Biotech ilisababisha ongezeko la kinga mwilini kwa haraka baada ya kutolewa kwa watu wapatao 700.

Tangazo hilo limewadia baada ya wataalamu kusema chanjo zilizotayarishwa katika mataifa ya Ulaya na nchini Marekani zimedhihirisha ufanisi baada ya majaribio.

Deta kuhusu chanjo tatu zilizofanyiwa utafiti nchini Ujerumani, Marekani na Urusi imeashiria kwamba zina uwezo wa asilimia 90 wa kuzuia maambukizi baada ya kufanyiwa majaribio miongoni mwa maelfu ya watu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *