CECAFA U 17 kuanza kutimua vumbi Jumapili

Michuano ya CECAFA  kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17 kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la Afcon mwaka ujao nchini Moroko itaanza rasmi Jumapili Disemba 13 Kenya wakifungua dimba kundini A dhidi ya Ethioipia kuanzia saa tisa alasiri katika uwanja wa Umuganda mjini Rubavu.

Mataifa 6 yanashiriki michuano hiyo baada ya Sudan Kusini kufurushwa mashindanoni Jumamosi kwa udanganyifu wa umri .

Wenyeji Rwanda watashuka uwanjani Jumatatu kukabana koo  na Tanzania katike mechi ya ufunguzi ya kundi B.

Sudan Kusini  waliofurushwa  mashindanoni kwa udanganyifu wa umri

Kenya watarejea uwanjani Jumatano dhidi ya Uganda  katika pambano la mwisho.

Tanzania maarufu kama Serengeti Boys ndio mabingwa watetzi wa kombe hilo la Cecafa walilonyakua mwaka jana kwa kuishinda Somalia kwenye mchuano wa fainali.

Kundi B linajumuisha wenyeji Rwanda ,Tanzania na Djibouti ambapo mechi za nusu fainali zitachezwa  Disemba 20 huku fainali yake ikisakatwa Disemba 22 huku timu mbili bora zikijikatia tiketi kupiga michuano ya AFCON mwezi Juni mwakani nchini Moroko.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *