CECAFA U 17 kuanza kutimua vumbi Jumamosi nchini Rwanda
Michuano ya kuwania kombe la Cecafa kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 17 itaanza Jumamosi hii mjini Kigali Rwanda huku mataifa manane yakiwania tiketi mbili za kucheza michuano ya Afcon mwaka ujao nchini Moroko.
Uganda watafungua ratiba ya mechi hiyo katika kundi B Jumamosi adhuhuri dhidi ya Sudan Kusini katika pambano la ufunguzi kuanzia saa sita kabla ya kuwapisha wenyeji Rwanda kutifua vumbi saa tisa unusu dhidi ya Tanzania.

Kenya watashuka uwanjani Jumapili kuvaana na Ethiopia katika kundi A .
Baade vijana wa Kenya wanaofunzwa na kocha Oliver Page watarejea uwanjani Disemba 15 dhidi ya Uganda ,kabla ya kuhitimisha ratiba dhidi ya Sudan Kusini tarehe 18.

Mashindano hayo yanayoandaliwa katika viwanja vya Rubavu na Kigali yatakamilika tarehe 22 huku timu mbili bora zikifuzu kupiga michuano ya Afcon bnchini Moroko Juni mwaka ujao.