Categories
Uchaguzi Tanzania 2020

Mbunge wa zamani wa Tanzania Godbless Lema atafuta hifadhi Kenya kwa kuhofia maisha yake

Aliyekuwa mbunge wa Arusha Urban nchini Tanzania Godbless Lema anatafuta hifadhi nchini Kenya kutokana na mizozo ya kisiasa huku akidai kuwa maisha yake yamo hatarini.

Mbunge huyo wa zamani alikesha usiku katika Kituo cha Polisi cha Kajiado baada ya kuripotiwa kukamatwa na maafisa wa Kenya katika sehemu ya Ilbisil kwenye barabara ya Namanga.

Lema, ambaye ameandamana na mkewe na watoto wao watatu amesema alikuwa amewasiliana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) kutafuta hifadhi akisema hataki kurejeshwa nchini Tanzania.

Kiongozi huyo wa zamani wa upinzani amesisitiza kuwa yeye si mhalifu anayekwepa sheria bali ni kiongozi anayekabiliwa na hatari ya kuuawa kwa kudumisha msimamo mkali wa kisiasa.

“Nimekimbilia Kenya kutafuta hifadhi ya maisha yangu,sio kwamba nimekimbia njaa ama nimekosa chakula lakini maisha yangu nay a familia yangu yamekuwa bora sana kwa wakati huu,” amesema Lema.

Wakili wake George Luchiri Wajackoyah, amesema hatua ya kuregeshwa kwao kwa mbunge huyo itakuwa ukiukaji wa haki zake na kusisitiza kuwa mteja wake anafaa kukabidhiwa kwa shirika la UNHCR.

Wakati uo huo, Shirika la Amnesty International humu nchini limetoa wito kwa serikali ya Kenya kutayarisha hati za kumhifadhi Godbless Lema kuambatana na sheria za kimataifa.

Shirika hilo limewataka maafisa wa humu nchini wasimrejeshe mwanasiasa huyo wa upinzani nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Irungu Houghton amesema kuwa maisha ya Lema yamo hatarini na kwamba kumkabidhi kwa serikali ya Tanzania huenda kukamfanya ateswe na kufungwa kwa sababu za kisiasa.

Irungu ameongeza kusema kuwa majukumu ya Kenya kuhusiana na sheria za kimataifa yanamruhusu yeyote anayetafuta hifadhi aingie humu nchini iwe ni kwa njia halali au bila kufuata taratibu zifaazo.

Masaibu ya Lema yanatokana na msako dhidi ya viongozi wa upinzani nchini Tanzania wiki moja baada ya Rais John Pombe Magufuli kuapishwa kwa hatamu ya pili ya miaka mitano kufuatia uchaguzi uliopingwa na upinzani.

Categories
Uchaguzi Tanzania 2020

Rais Magufuli aapishwa kuongoza Tanzania kwa muhula wa pili

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ameapishwa kuiongoza taifa hilo kwa muhula wa pili.

Rais Magufuli alitetea wadhifa wake baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu ulioandaliwa nchini humo tarehe 28 mwezi Oktoba mwaka huu.

Tume ya uchaguzi nchini Tanzania ilitangaza kuwa Magufuli alipata kura 12,516,252 hii ikiwa ni asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa.

Mwaniaji kiti hicho cha Urais wa upinzani Tundu Lissu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, alikuwa wa pili kwa kuzoa jumla ya kura 1,933,271.

Hata hivyo upinzani nchini Tanzania ulidai kuwa shughuli hiyo ilikumbwa na udanganyifu huku ukitaka zoezi hilo kurudiwa upya.

Raia wa Tanzania walifika katika uwanja wa michezo wa Dodoma, kuhudhuria sherehe hizo kuanzia saa kumi na mbili alfajiri.

Mataifa 12 yaliwakilishwa katika sherehe hiyo sawia na wawakilishi kutoka muungano wa Afrika AU.

Kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo NEC, kati ya watu 29,754,699 waliojiandikisha kupiga kura, ni watu 15,91950 waliojitokeza kupiga kura hizo.

Awamu hii ya pili ya Magufuli itakamilika mwaka 2025.

Categories
Uchaguzi Tanzania 2020

Washukiwa wa maandamano ya kupinga matokeo ya Urais Tanzania waachiliwa huru

Polisi nchini Tanzania wamewaachilia kwa dhamana viongozi wote wa upinzani waliokamatwa kwa madai ya kufanya maandamano bila kibali.

Wanasiasa hao ni pamoja na mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, Freeman Mbowe, na kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.

Wote walishtakiwa kwa makosa ya kuandaa maandamno kinyume cha sheria na makosa ya jinai.

Baadhi ya wanasiasa hao walitiwa nguvuni siku ya jumapili.

Upinzani umeitisha mfululizo wa maandamano ya umma kulalamikia matokeo ya uchaguzi wa urais wa wiki iliopita, ambapo Rais John Pombe Magufuli alishinda kwa aslimia 84 ya kura hizo.

Upinzani umekataa matokeo ya uchaguzi huo na kusema una ushahidi kwamba kulifanyika udanganyifu kwenye uchaguzi huo.

Hata hivyo, polisi wameshtumu wafuasi wa upinzani kwa kuteketeza masoko na vituo vya mafuta ya petrol wakati wa maandamano ambayo yalipangiwa kuanza Jumatatu lakini hayakufanywa.

Siku ya Jumatatu, mgombea urais wa upinzani Tundu Lissu alitiwa nguvuni kwa muda lakini akaachiliwa baadaye kutokana na sababu za kiafya.

Categories
Uchaguzi Tanzania 2020

Mwenyekiti wa CHADEMA, Tanzania, akamatwa kwa madai ya kupanga ghasia

Maafisa wa polisi nchini Tanzania wamemtia nguvuni mwenyekiti wa chama cha upinzani CHADEMA, Freeman Mbowe kwa madai ya kupanga gasia za baada ya uchaguzi nchini humo.

Polisi wamesema Mbowe alikamatwa pamoja na viongozi wengine wawili wa chama hicho kwa madai ya kupanga ghasia wakati wa maandamano dhidi ya matokeo ya uchaguzi yaliyozozaniwa.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa Ijumaa iliyopita, mwaniaji wa chama cha CCM, Dkt. John Pombe Magufuli alishinda kwa asilimia 84 ya kura zilizopigwa.

Hata hivyo, upinzani unadai uchaguzi huo ulikumbwa na wizi wa kura na kuwahimiza raia kuandamana kupinga matokeo yake.

Mwaniaji wa upinzani Tundu Lissu anadai mawakala wa chama chake walizuiwa kuingia ndani ya baadhi ya vituo vya kupigia kura ambako masanduku ya kura yalivurugwa.

Mwishoni mwa juma, viongozi wa vyama vya CHADEMA na ACT-Wazalendo waliwarai wafuasi wao kuandamana kwa amani kupinga matokeo hayo.

Hata hivyo polisi wamedai taarifa za kijasusi zinaashiria kuwa waandamanaji hao walinuia kuteketeza masoko na vituo vya petroli.

Categories
Uchaguzi Tanzania 2020

Vyama vya upinzani nchini Tanzania vyataka uchaguzi mkuu urudiwe upya

Vyama viwili vikuu vya upinzani nchini Tanzania vimeshinikiza kuandaliwa kwa uchaguzi mpya baada ya kupinga uchaguzi wa urais wa  juma lililopita vikisema ulikumbwa na udanganyifu.

Vyama hivyo vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kile cha Alliance for Change and Transparency-Wazalendo (ACT-Wazalend),kwenye mkutano wa pamoja na wanahabari pia vilitoa wito wa maandamano kuanzia siku ya Jumatatu.

Rais John Magufuli alitangazwa kuwa mshindi kwenye uchaguzi uliofanyika siku ya Jumatano akiwa amepata asilimia 84 ya kura.

Chama cha CHADEMA kimedai kwamba masanduku ya kura yalivurugwa baada ya maajenti wake kuzuiwa kuingia kwenye vituo vya kupigia kura.

Kiongozi wa cha chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe alsiema kuwa uamuzi huo unahusiana na kile alichokitaja kuwa hatima ya nchi hiyo.

Mwaniaji urais wa chama cha CHADEMA Tundu Lissu alipata asilimia 13 ya kura. Mkuu wa tume ya kitaifa ya uchaguzi, Semistocles Kaijage, alisema kwamba madai ya karatasi bandia za kura hayana msingi. Ujumbe wa uchunguzi wa jumuiya ya Afrika mashariki ulisema kuwa uchaguzi huo ulitekelezwa kwa njia ifaayo.

Hata hivyo ubalozi wa marekani jijini Dar es Salaam ulisema kuwa kasoro pamoja na tofauti kubwa katika asilimia ya kura za mshindi zinaibua shauku kuhusiana na uadilifu wa matokeo hayo.

Categories
Uchaguzi Tanzania 2020

Magufuli achaguliwa tena Rais wa Tanzania licha ya madai ya udanganyifu katika uchaguzi huo

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amechaguliwa tena kuiongoza Tanzania kwa kipindi kingine cha mika mitano katika uchaguzi mkuu ulioandaliwa siku ya Jumatano.

Kulingana na tume ya uchaguzi nchini Tanzania NEC, Magufuli alipata kura 12,516,252 na kumbwaga mwaniaji wa upinzani Tundu Lissu aliyepata Kura 1,933,271.

Licha ya kuwa watu 29,754,699 walijiandikisha kuwa wapiga kura, ni watu 15,91950 waliojitokeza kupiga kura hizo siku ya Jumatano kwa mujibu wa tume ya uchaguzi nchini Tanzania.

Magufuli ametangazwa mshindi katika uchaguzi uliotajwa kukumbwa na udanganyifu,huku mgombea urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Tundu Lissu akidai mawakala wa upinzani katika uchaguzi huo hawakuruhusiwa kuingia katika vituo vya kupiga kura.

Hata hivyo madai ya Lissu hayakuungwa mkono na aliyekuwa Rais wa Burundi Silvestre Ntibantunganya aliyesema uchaguzi huo ulifuata taratibu zifaazo.

Ntibantunganya ambaye ni mwenyekiti wa ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi kutoka Afrika Mashariki, alivitaka vyama vya kisiasa nchini humo kutumia sheria zilizopo kuwasilisha malalamishi yao.

Na katika visiwa vya Zanzibar, mgombea urais wa chama cha Mapinduzi Hussein Mwinyi alitangazwa mshindi kwa kupata asilimia 76 ya kura zilizopigwa.

Mpinzani wake wa Karibu Maalim Seif Sharif wa chama cha Alliance for Change and Transparency-Wazalendo (ACT-Wazalendo), alipata asilimia 19 ya kura zote zilizopigwa.

 

Categories
Uchaguzi Tanzania 2020

Dkt Hussein Ali Hassan Mwinyi wa CCM ashinda Urais wa Zanzibar

Dkt Hussein Ali Hassan Mwinyi ndiye  Rais mpya wa awamu wa 8 kisiwani Zanzibar kupata kuta 380,402  kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM sawa na asilimia 76.27.

Matokeo hayo yametangazwa Alhamisi jioni na tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar.

Katika hotuba yake baada ya kutangazwa mshindi ,Dkt Miwnyi aliwapongeza wapinzani wake na kutoa fursa kwa maridhiano na mshikamano wa kitaifa.

Dkt Mwinyi ni mwanawe Rais wa awamu ya pili ya muungano wa Tanzania   Ali Hassan Mwinyi.

Chama cha CCM tayari kimezoa viti 136  vya Ubunge kati ya viti vyote 264 ikiwa asilimia 75 kikifuatwa na CHADEMA iliyo na asilimia 20 ya wabunge huku ACT Wazalendo na vyama vingine wakigawana asilimia zilizosalia ikiwa ni 2 na tatu mtawalia .

Categories
Burudani Uchaguzi Tanzania 2020

Prof Jay apoteza ubunge wa Mikumi kwa mpinzani wa CCM

Msanii maarufu wa nyimbo za Hip Hop Tanzania Bara Joseph Haule maarufu kama Prof Jay amepoteza ubunge wa Mikumi  baada ya kubwagwa na mpinzani wa  Chama cha Mapiunduzi CCM.

Prof jay akigombea kiti hicho kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) alipata kura 17,375 dhidi ya  mgombea wa chama tawala cha CCM Denis Lazaro aliyeibuka mshindi kwa kupata kura 31,411 .

Prof Jay ameliongoza Jimbo la Mikumi kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kushinda kwenye Uchaguzi uliopita mwaka 2015 .

Uchaguzi mkuu wa Tanzania uliandaliwa Jumatano huku shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea kwa maeneo mengi nchini humo.

Categories
Uchaguzi Tanzania 2020

Tundu Lissu: Uchaguzi mkuu wa Tanzania ulikumbwa na udanyanyifu

Mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia cha Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania Tundu Lissu, amesema uchaguzi mkuu ulioandaliwa Jumatano nchini humo ulikumbwa na udanganyifu.

Mgombea huyo wa urais wa upinzani alidai kuwa mawakala wa upinzani hawakuruhusiwa kuingia katika vituo vya kupiga kura.

Lissu ametoa wito kwa jumuiya za kikanda zikatalie mbali matokeo ya uchaguzi wa Tanzania aliyoyataja kuwa haramu.

Hata hivyo tume ya uchaguzi nchini Tanzania imepuuzilia mbali madai hayo ya Lissu ikiyataja yasiyo na msingi wowote.

Mkuu wa tume hiyo ya uchaguzi Semistocles Kaijage, alisema madai kwamba kulikuwa na karatasi bandia za kupiga kura si ya ukweli.

Vyombo vya habari nchini Tanzania viliripoti kuwa shughuli ya upigaji kura Tanzania bara na visiwani Zanzibar ilikuwa ya Amani.

Rais wa nchi hiyo John Magufuli anawania awamu ya pili katika uchaguzi huo.

Categories
Uchaguzi Tanzania 2020

Watanzania wafanya maamuzi ya Kura

Zaidi ya wapiga kura milioni 29 waliojiandikisha wamejitokeza kupima kura mapema Jumatano katika maeneo yote nchini Tanzania huku kukiripotiwa kukatizwa kwa huduma za mitandao na Internet nchini humo.

Mitandao kadhaa ya kijamii ikiwemo Whatsapp na Twitter imefungwa kwa wengi  nchini Tanzania kuanzia mapema Jumanne huku pia kukiripotiwa na ghasia baada ya polisi kumkamata kiongozi wa upinzani kutoka kisiwani Zanzibar.

Rais John Pombe Magufuli anawania muhula wa pili afisini  kwa  tiketiti ya Chama Cha Mapinduzi CCM huku akipingwa na wagoembea wengine 15 akiwemo Tundu Lisu wa  Chadema .