Categories
Michezo

Chelsea iliongoza kwa kutumia hela nyingi kwa usajili wachezaji

Timu za ligi kuu Uingereza zilitumia pauni bilioni 1 nukta 2 kwa usajili wa wachezaji  wakati wa dirisha la usajili lililofungwa  usiku wa Oktoba 5 mwaka huu.

Kiwango hiki kina upungufu wa pauni milioni 160 kutoka kwa kiwango kilichotumika msimu uliopita  lakini ni pauni milioni 70 zaidi ya kiwango kilichotumika mwaka 2016.

Chelsea ndio timu iliyoptumia hela nyingi kwa usajili ikiwa pauni milioni 226 nukta 1 kwa kuwaleta wachezaji  wakiwemo Timo Werner pauni milioni 45m , Hakim Ziyech pauni milioni 37m,Edouard Mendy pauni milioni 22 na Ben Chilwell pauni milioni 50m pamoja na Kai Havertz aliyenunuliwa kwa pauni  milioni 70.

Manchester City ilikuwa ya pili kwa kutumia  pauni milioni 147 ikiwaleta Nathan Ake kwa pauni milioni 41m , Ferran Torres kwa pauni milioni 37.

.

Aston Villa ilitumia pauni milioni 85 ikifuatwa na Leeds United kwa pauni  milioni 84.

Categories
Michezo

Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu kung’atuliwa

Rais wa kilabu cha Barcelona  Josep Maria Bartomeu huenda akang’atuliwa mamlakani  kupitia kura ya kutokuwa na imani naye baada hoja hiyo ya kumbandua kupata zaidi ya kura 16,500 zinazohitajika .

Hoja ya kumbandua kinara huyo ilianza mwezi Agosti  wakati wa zogo kuhusu uhamisho wa mchezaji nyota Lionel Messi .

Jordi Farre, ambaye anataka kumrithi Bartomeu aliwasilisha hoja ya kukosa imani na kinara wa sasa akisema kuwa wamekuwa miaka mingi ya  usimamizi duni  kwenye timu hiyo .

Zaidi ya wanachama 20,000 walisaini hoja hiyo ya kukosa imani na usimamizi wa sasa tangu mwezi uliopita

Barca sasa watahitajika kupanga tarehe mpya ya kuandaa kura ya maoni  ndani  ya siku 20 zijazo huku shughuli hiyo ikiwashirikisha wanachama 154,000 amnbapo ambapo asilimia 66.6 ya wanachama wanapaswa kuunga mswaada huo ili kumng’atua Bartomeu.

Endapo kura hiyo itafaulu timu hiyo inatarajiwa kufanya uchaguzi wa kumtafuta rais mpya huku Farre akiwa miongoni mwa wanaowania kiti hicho pamoja na  Victor Font na  Joan Laporte.

Yamkini kuwa Bartomeu huenda akajiuzulu kabla ya kura hiyo huku muhula wake wa kuhudumu ukikamilka mwaka ujao   .

Categories
Michezo

Joshua Cheptegei awinda rekodi ya dunia ya mita 10000

Mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za mita 5000 Joshua Cheptegei atalenga kuvunja rekodi ya dunia ya mita 10000 atakaposhiriki mashindano ya NN Valencia  World Record Day nchini Uhispania Jumatano usiku.

Cheptegei  aliye na umri wa miaka 22  analenga kuvunja rekodi ya dakika 26 sekunde 17 nukta 53 iiliyoandikishwa na  Kenenisa Bekele wa Ethiopia Miaka 15 iliyopita,ikiwia ndiyo rekodi iliyodumu kwa muda mrefu zaidi upande wa wanaume.

Cheptegei atawekewa kasi na wanariadha  kadhaa wakiwemo Nicholas Kimeli wa Kenya aliyeshinda mbio za mita 5000 katika mashindano ya  Kip Keino Classic .

Wapinzani wa Cheptegei watakuwa Mganda mwenza Victor Kiplangat  na Shadrack  Kipchirchir wa Marekani .

Bingwa huyo wa dunia katika mita 10000 aliandikisha rekodi mpya ya dunia  katika mita 5000 mjini Monaco Ufaransa katika mashindano ya Monaco Diamond league na kuweka rekodi ya dakika 12 sekunde 35 nukta 36 mwezi Agosti  akivunja ile ya Haille Gebresselasie iliyodumu miaka 16 ya dakika 12 sekunde 37 nukta 35 .

Letesnet Gidey wa Ethiopia

Mshindi wa nishani ya fedha ya dunia katika mita 10000 Letesenbet Gidey wa Ethiopia atawania kuvunja rekodi ya wanawake ,  iliyoandikishwa na mwethiopia mwenza Tirunesh Dibaba  ya dakika 14 sekunde  11 nukta  15 mwaka 2008.

Bingwa wa dunia na mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mita 3000 kuruka viunzi na maji Beatrice Chepkoech atakuwa miongoni mwa wapiga kasi katika mbio za akina dada Jumatano usiku.

 

Categories
Michezo

Zambia kuwasili Alhamisi kwa mechi dhidi ya Kenya

Mabingwa wa Afrika mwaka  2012 Zambia maarufu kama Chipolopolo wanatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi tayari kwa pambano la kirafiki dhidi ya wenyeji Harambee Stars Ijumaa hii Oktoba 9 katika uwanja wa Taifa wa Nyayo.

Zambia sawa na Kenya itakosa huduma za wachezaji wengi wa kulipwa waliobanwa kusafiri kutokana na masharti makali ya ugonjwa wa Covid 19 na watacheza pambano la Ijumaa jioni na kisha kuabiri ndege hadi Afrika Kusini waliporatibiwa kupiga mchuano wa tatu wa kujinoa makali dhidi ya Bafanabafana Jumapili jioni.

Mkufunzi wa Zambia  Milutin ‘Micho’ Sredojevic aanatarajiwa kwuatumia wachezaji wengi wa nyumbani katika mechi hizo za kirafiki huku wakijiandaa kukabiliana na Botswana katika mechi mbili za kundi H mwezi ujao kufuzu kwa Kombe la Afcon mwaka ujao dhidi ya Botswana.

 

 

Categories
Michezo

Derby ya Simba na Yanga yaahirishwa

Derby ya Kariakor baina ya timu za Simba na Yanga mchuano wa ligi kuu Tanzania bara uliokuwa uchezwa Oktoba 18 imesogezwa mbele hadi Novemba 7 katika uwanja wa Benjamin Mkapa Daresalaam.

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania limelazimika kuchukua hatu hiyo kutokana na vikwazo vilivyopo vya usafiri katika baadhi ya mataifa kuhusu ugonjwa wa Covid 19 ,na huenda timu hizo zikaathirika kutokana na kukosa baadhi ya wachezaji wao tegemeo.

Yanga watakuwa wenyeji wa Derby hiyo.

Waraka wa bodi inayoendesha ligi kuu ya Tanzania bara Vodacom
Categories
Michezo

Hellen Obiri kukosa kutetea taji ya dunia ya mbio za Nyika mwaka ujao

Bingwa wa dunia katika mbio za mita 5000 Hellen Obiri amesema kuwa hatatetea taji yake ya dunia ya mbio za nyika mwaka ujao nchini Australia badala yake ataangazia kutwaa dhahabu ya Olimpiki ambayo imemkwepa kwa muda mrefu kabla ya kuhamia mbio  barabarani na marathon.

Mwanariadha  huyo aliye na umri wa miaka 31 na ,ambaye ni bingwa wa jumuiya madola , amesema kuwa atakosa kwenda mjini Barthurst Australia kwenye  makala ya 44 ya mashindano ya dunia ya mbio za nyika mwaka ujao kutokana na hali anga iliyo Australia ambayo huenda ikaathiri matayarisho yake kwa michezo ya Olimpiki.

‘’Sitaenda Australia Machi 2021 ,kutetea taji yangu ya dunia ya mbio za nyika ,nataka kuangazia   michezo ya Olimpiki ambapo nitaketi chini na meneja wangu kuamua iwapo nitashiriki mita 5000 au 10000 au zote mbili mjini Tokyo Japan mwaka ujao’’ Akasema Obiri

Obiri ambaye ni afisa wa Kdf alinyakua dhahabu ya dunia katika mbio za nyika mwaka uliopita mjini Aarus Denmark.

Obiri akiwa katika mzunguko wa mwisho wa mita 5000 katika mashindano ya Kip Keino Classic Jumamosi iliyopita

Mwanariadha huyo aliyesajili muda wa kasi katika mikondo ya Monaco na Brussels katika mashindano ya diamond league mwezi Agost,i ametangaza kuwa kwa sasa atachukua mapumziko kabla ya kureja uwanjani mwaka ujao.

Baada ya kushinda nishani ya fedha ya Olimpiki ,Obiri anaazimia kunyakua dhahabu ya olimpiki mwaka huu mjini Tokyo Japan ,kabla   ya kuhamia mashindano ya barabarani, lakini ameahirisha mipango yote hadi mwaka ujao kufuatia kuahirishwa kwa olimpiki kutokana na janga la Covid 19.

Obiri alifunga mwaka huu kwa njia ya kipekee kwa kushinda mbio za mita 5000 katika mashindano ya Kip Keino Classic kwenye  uwanja wa Taifa wa Nyayo Jumamosi iliyopita .

 

Categories
Michezo

Maandamano kupinga kuchelewesha ujenzi wa uwanja wa Dandora

Wapenzi wa michezo mtaani Dandora waliandama Jumanne kupinga ucheleweshwaji kukamilisha ujenzi wa uwanja wa Dandora uliokuwa ukijengwa na serikali ya kaunti ya Nairobi.

Ujenzi wa uwanja huo mpya wa Dandora ulisimamishwa kutokana na kesi ya ufusadi inayomkabili Gavana Mike Sonko.

Wakandarasi walisitisha ujenzi na kuacha vifaa vya ujenzi wakati uwanja  huo ulikuwa umekaribia asilimia 80 kukamilika wakati tume ya kukabiliana na ufisadi EACC  ilipositisha shughuli hiyo kwa madai ya ufujaji wa pesa .

uwanja huo utakuwa na uwezo wa kumudu mashabiki wapatao 3000 utakapokamilika.

 

 

Categories
Michezo

Randy Waldrum ateuliwa kuwa kocha wa Super Falcons

Randy Waladrum amateuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria  Super Falcons.

The Falcons haijakuwa na mkufunzi tangu Thomas Dennerby afurushwe kufuatia mataokeo mabovu katika fainali za kombe la dunia mwaka 2019 nchini Ufaransa.

Waldrum,kiungo wa zamani wa Marekani na pia alikuwa kocha wa timu ya   ya Marekani kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 23 na kuhudumu pia kama kocha wa U Trinidad and Tobago baina ya mwaka  2014 na  2016.

Waldrum anatarajiwa kujiunga na kapteini  zamani wa Nigeria  Ann Chiejine, ambaye  ni naibu wa kwanza wa kocha huku  Wemimo Mathew Olanrewaju akiwa msaidizi wa pili  Coach naye Auwar Bashir Makwalla akiwa mkufunzi wa makipa.

Categories
Michezo

Soko la Ulaya lafungwa huku Thomas Party akijiunga na Arsenal na Man U yamnasa Cavani

Soko la kununua na kuuza wachezaji lilifungwa rasmi jumatatu usiku huku timu mbalimbali zikifanya usajili wa dakika  za mwisho.

Kiungo wa Ghana Thomas Partey ajiunga na Arsenal kwa pauni milioni 45 kikiwa kiwango cha juu Zaidi katika siku ya mwisho ya soko.

Partey alisaini mkataba wa muda mrefu na The gunners baada ya kupasi vipimo vya ki afya na ndiye mwanadinga wa 7 kutua Emirates msimu huu ambapo atavalia jezi nambari 18 .

Partey atakuwa akipokea ujira wa pauni 260,000 kwa wiki akiwa London.

Manchester United kwa upande wake ilipata huduma za mshambulizi  Edinson Cavani kwa kandarasi ya mwaka mmoja baada ya kuigura Psg mwishoni mwa msimu uliopita.

Canavi amecheza jumla ya michuano 556 na kufunga mabao 341 na analeta tajriba katika safu ya mbele ya United iliyo na chipukizi Marcus Rashford na Maison Greenwood na Athony Martial kumaanisha kuwa Odeon Ighalo aliye old traford kwa mkopo ataruhisiwa kureje Uchina Januari mwakani.

Beki Cris Smalling aliigura Man u na kujiunga na As Roma kwa pauni milioni 18 kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kuwa Roma kwa mkopo .

Mashetani wekundu pia walifanikiwa kumsajili beki pemebeni kuhsoto Alex Telles kutoka Fc Porto ya Ureno kwa pauni milioni 15 nukta 4.

Pia wing’a wa Everton Theo Walcot amerejea katika timu yake ya utotoni Southampton kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.

Licha ya soko kufungwa kwa uhamisho barani Ulaya ,ununuzi na uuzaji wachezaji katika ligi zote za Uingereza ungali wazi hadi Oktoba 16

Ufuatao ni uhamisho wa wachezaji katika timu kadhaa katika ligi kuu Uingereza

Wachezaji Waliojiunga na Arsenal

Willian  kutoka Chelsea kwa uhamisho usio wa malipo

George Lewis  kutoka Fram Larvik

Tim Akinola kutoka Huddersfield uhamisho usio wa malipo

Salah-Eddine kutoka Feyenoord uhamisho usio wa malipo

Jonathan Dinzeyi kutoka Tottenham Spurs uhamisho wa bure

Pablo Mari kutoka Flamengo

Cedric Soares kutoka Southampton

Gabriel kutoka Lille

Dani Ceballos ambaye ameongeza mkataba wa mkopo kutoka Real Madrid

Alex Runarsson kutoka Dijon

Thomas Partey kutoka Atletico Madrid

 Wachezaji waliojiunga na Chelsea

Timo Werner kutoka RB Leipzig

Hakim Ziyech kutoka Ajax

Ben Chilwell kutoka Leicester

Malang Sarr kutoka Nice

Thiago Silva kutoka PSGs

Kai Havertz kutoka Bayer Leverkusen

Edouard Mendy kutoka Rennes

Wachezaji waliotua Liverpool

Konstantinos Tsimikas kutoka Olympiacos

Thiago Alcantara kutoka Bayern Munich

Diogo Jota kutoka Wolves

Wachezaji waliojiunga na Manchester City

Pablo Moreno kutoka Juventus

Ferran Torres kutoka Valencia

Nathan Ake kutoka AFC Bournemouth

Scott Carson kutoka Derby County kwa mkopo

Ruben Dias kutoka Benfica

Wachezaji waliotua Tottenham Hotspur

Pierre-Emile Hojbjerg kutoka Southampton

Joe Hart kutoka Burnley

Matt Doherty kutoka Wolves

Sergio Reguilon kutoka Real Madrid

Gareth Bale kutoka Real Madrid kwa mkopo

Carlos Vinicius kutoka Benfica kwa mkopo

 

 

 

 

Categories
Michezo

Mechi ya Harambee Stars dhidi ya Zambia kuendelea ilivyoratibiwa

Harambee Stars imeruhusiwa kuendelea mbele na matayarisho kwa mchuano wa kujipima nguvu dhidi ya Chipolopolo kutoka Zambia Ijumaa hii.

Akitoa hotuba yake jumatatu jioni ,katibu mwandamizi katika wizara ya afya Dr Rashid Aman amesema kuwa wameafikiana na wizara ya michezo kuwaruhusu wachezaji wa Harambee Stars kuendelea  mbele na maandailizi kwa mchuano huo utakaosakatwa katika uwanja wa taifa wa Nyayo.

Pambano la Ijumaa litakuwa la kwanza kwa Harambee Stars mwaka ingawa wachezaji na maafisa wa timu hiyo watalazimika kuzingatia masharti ya serikali kuhusu ugonjwa wa Covid 19.

Awali mapema Jumatatu wachezaji na maafisa wa Harambee stars walizuiwa kuingia uwanjani Kasarani kuanza mazoezi kufuatia agizo la serikali la kutoruhusu mchezo wa soka kurejelewa.

Stars itakosa huduma za wachezaji wa kulipwa wakiwemo Ayum Timbe Masika,Victor Wanyama,Arnold Origi an mshambulizi Michael Olunga waliozuiwa kusafiri kutokana na masharti makali ya usafiri kwa mataifa wanayopiga soka .

Kwa upande wao Zambia wanaofunzwa na kocha Milutin Sredejovic pia watokosa wachzaji Patson Daka na  Erick Mwepu wanaosakata soka ya kulipwa katika kilabu cha Red Bull Salzburg nchini Austria .