Categories
Michezo

Mamelodi na Belouizdad kuchuana Benjamin Mkapa jijini Dare salaam

Shirikisho la kandanda Afrika limetangaza kuwa mechi ya pili ya kundi B kuwania kombe la ligi ya mabingwa Afrika kati ya mabingwa wa Ageria CR Belouizdad ya Algeria na mabingwa wa Afrika Kusini Mamelodi Sundowns itachezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa mjini Daresalaam Tanzania tarehe 28 Februari.

Mchuano huo ulikuwa upigwe mjini Algiers Algeria lakini ukalazimika kuhamishwa baada ya serikali ya Algeria kupiga marufuku safari zote za kuingia nchini humo kama njia ya kuzia msambao wa ugonjwa wa Covid 19.

Shirikishp la soka Tanzania TFF limeidhinisha pambano hilo kuandaliwa nchini humo.

CAF pia imengaza kuwa mechi ya kundi C kati ya Wydad Casablanca ya Moroko na Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini itachezwa tarehe 28 mwezi Februari katika uwanja wa 4TH August mjini Ouagadogou Burkina Faso baada ya kuidhinishwa na shirikisho la kandanda nchini Burkina Faso.

Mechi za mzunguko wa pili hatua ya makundi kuwania ligi ya mabingwa Afrika zitapigwa kati ya Ijumaa na Jumamosi hii.

Categories
Michezo

Mabingwa watetezi RS Berkane kuzindua uhasama na Kabylie ya Algeri kombe la shirikisho

Mabingwa watetezi wa kombe la shirikisho la Soka Afrika RS Berkane kutoka Moroko wamejumuishwa kundi B pamoja na vigogo wa Algeria Js Kabylie kwenye droo ya kombe hilo iliyoandaliwa Jumatatu alasiri mjini Cairo Misri.

Timu nyingine kundi hilo ni Cotton Sport ya Cameroon na NAPSA Stars ya Zambia iliyoibandua Gor Mahia.

Berkane wataanza kutetea kombe hilo tarehe 10 mwezi Machi wakiwaalika NAPSA Stars,kabla ya kuzuru Yaounde kupimana nguvu na Cotton Sport ya Cameroon tarehe 17 Machi,kisha iwaalike Js Kabylie ya Algeria April 4, kuzuru Algeria kwa mechi ya marudio tarehe 11 mwezi wa nne na kisha kupiga ziara ya Lusaka kuchuana na NAPSA tarehe 25 na kuhitimisha ratiba tarehe 28 April kwa kuwaalika NAPSA.

Kundi A linajumuisha vilabu vya Enyimba kutoka Nigeria,Entete Setif ya Algeria,Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Ahli Bengazi ya Libya.

Asc Jaraaf kutoka Senegal imejumuishwa kundi C pamoja na Salitas ya Burkina Faso,CS Faxien ya Tunisia na mshindi wa mechi ya mchujo baina ya Etoile Du Sahel ya Tunisia na Young Buffaloes ya Swaziland.

Pyramids ya Misri iliyoshindwa kwenye fainali ya mwaka uliopita imo kundi D pamoja na Raja Casablanca ya Moroko,Nkana Rangers kutoka Zambia na mshindi wa pambano la mchujo kati ya Premeiro de Agosto ya Angola na Namungo kutoka Tanzania.

Kombe la shirikisho Afrika

Droo kamili:-

Kundi A
Enyimba-Nigeria
Entete Setif-Algeria
Orlando Pirates-South Africa
Ahli Bengazi-Libya

Kundi B
RS Berkane-Morocco
NAPSA Stars-Zambia
JS Kabylie-Algeria
Cotton Sport-Cameroon

Kundi C
Asc Jaraaf-Senegal
Salitas – Burkina Faso
CS Faxien – Tunisia
Mshindi kati ya Etoile Du Sahel ya Tunisia na Young Buffaloes ya Swaziland.

Kundi D
Pyramids – Egypt
Raja Casablanca – Morocco
Nkana Rangers-Zambia
mshindi wa pambano la mchujo kati ya Premeiro de Agosto ya Angola na Namungo kutoka Tanzania.

Mshindi wa kombe hilo atatuzwa dola milioni 1 nukta 25.

Categories
Michezo

Kenya yalenga kufanya vyema FIBA Afrobasket asema kocha Milz

Kocha wa timu ya Kenya ya mpira wa kikapu kwa wanaume Liz Mils amesema analenga kusajili matokeo mazuri kwenye mashindano ya kombe la bara Afrika mjini Kigali Rwanda mwezi Agosti mwaka huu.

Mils ambaye ndiye kocha wa kwanza wa kike kuifuzisha timu ya wanaume kwa mashindano ya FIBA Afrobasket ,amekiri kuwa vijana wake walishindwa na Msumbiji katika mchuano wa mwisho wa kundi B Jumapili kutokana na uchovu baada ya kustahimili ukinzani mkali kabla ya kuilemea Angola pointi 74-73 mjini Yaounde Cameroon na kutinga michuano ya Afrika kwa mara ya kwanza baada ya ya miaka 28.

“Katika mechi ya leo dhidi ya Msumbiji vijana wangu walikuwa wamechoka kufuatia ushindi dhidi ya Angola timu ambayo naiheshimu sana,kikubwa kwetu sasa ni kujitayarisha vizuri ili tusajili matokeo bora mjini Kigali Rwanda”akasema Milz

Milz amesema wanawake wana uwezo wa kufanya vyema na wanapaswa kupewa fursa kuziongoza timu za wanaume.
“Ni wakati mwakafak ambapo pia wanawake wanastahili kupewa nafasi ya kuongoza timu za wanaume,na sisi kama wanawake tunaondoa vikwazo”akaongeza Milz

Kenya ilimaliza ya tatu katika kundi B baada ya kupoteza kwa Senegal na Msumbiji na kuishinda Angola .

Makala ya 30 ya mashindano ya FIBA Afrobasket yataandaliwa Kigali Rwanda baina ya Agosti 24 na Septemba 5 mwaka huu.

Categories
Michezo

Gor Mahia watajilaumu kwa kushindwa kufuzu hatua ya makundi

Mabingwa wa ligi ya Kenya Gor walipoteza uongozi wa mabao 2-1 ugenini katika uwanja wa Heroes mjini Lusaka dhidi ya NAPSA All Stars na kutoka sare ya magoli 2-2 Jumapili jioni matokeo yaliyozima ndoto ya Gor kutinga hatua ya makundi ya kombe la shirikisho la soka Afrika kwa mara ya pili katika historia.

Gor maarufu kama Kogalo walikuwa waliongoza mabao 2-1 kufikia mapumzikoni ,magoli yao yakipachikwa wavuni na Samuel Onyango kunako dakika ya 17 kabla ya Austin

Banda kuwarejesha wenyeji mchezoni dakika moja baadae naye Clifton Miheso akatikisa wavu kwa goli la pili dakika ya 20.

Kipindi cha pili kilisalia kigumu kwa timu zote kabla ya mwamuzi kuwapa wenyeji penati ya dakika ya 96 iliyofungwa na Emmanuel Mayuka na kuwafuzisha Napsa kwa hatua ya makundi huku Gor wakifeli kuingia hatua hiyo.

Kabla ya mchuano huo Kogalo walikumbwa na masaibu si haba ikiwemo mgomo wa wachezaji na kusafiri kuelekea Lusaka wakiwa wamechelewa.

Ni funzo kwa wasimamizi kujaribu kuweka mambo sawa kwenye timu hiyo ili irejelee matokeo mazuri .

Categories
Michezo

Jepchirchir na Olunga watawazwa wanaspoti bora SOYA

Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya nusu marathon Peres Jepchirchir na mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga walitawazwa wanamichezo bora wa mwaka uliopita katika makala ya 17 ya tuzo za SOYA yaliyoandaliwa mjini Naivasha Jumamosi usiku.

Jepchirchir alitawazwa mshindi baada  ya kuwa na msimu wa akufana aliposhinda taji ya pili ya dunia ya nusu marathon mjini Gydinia Poland huku pia akivunja rekodi ya dunia wiki 6 baada ya kuivunja katika mashindano ya Prague half marathon.

Jepchirchir aliweka muda wa dakika 57 na sekunde 32  ikiwa rekodi ya dunia ya wanawake pekee kabla ya kufunga msimu kwa njia ya kipekee akiandikisha muda wa tano wa kasi katika mbio za marathon aliposhinda makala ya 40 ya mbio za Valencia marathon wa saa 2 dakika 17 na sekunde  16 ikiwa mara yake ya kwanza kutimka marathon.

Bingwa  huyo  mara 2 wa dunia katika mbio za nusu marathon alimshinda Christine Ongare, aliyeshinda nishani ya shaba kwenye mashindano ya kufuzu kwa michezo ya Olimpiki na Faith Ogalo wa Taekwondo .

Upande wake Olunga ,alikuw ana msimu wa kufana mwaka jana akiibuka mfungaji bora kwa magoli 27 katika ligi kuu ya Japan pamoja na kutuzwa mchezaji bora kwenye ligi hiyo ya J1 league na kuwa mchezaji wa kwanza mwafrika kushinda tuzo hiyo akiwa na klabu ya Kashiwa Reysol.

Olunga aliwashinda bondia Nick Okoth, aliyenyakua fedha katika mashindano ya Afrika kufuzu ka michezo ya Olimpiki na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya nusu marathon Kibiwott Kandie .

Orodha kamili ya washindi ni kama ifuatayo:-

Outstanding Sportswoman living with a disability: Nancy Chelangat

Outstanding Sportsman living with a disability: Onesmus Munyao

Outstanding Sportswoman: Peres Jepchirchir

Outstanding Sportsman: Michael Olunga

Hall of Fame: Ben Jipcho, Rose Naliaka

Community Hero: Shadrack Wambui

Corporate Social Responsibility: Fidelis Njoki

Innovation: Dominic Ndigiti

Resilience– Sportsman living with a disability: Henry Wanyoike

Resilience– Sportsman: Daniel Komen

Tuzo ya SOYA ilianzishwa miaka 17 iliyopita na Rais wa kamati ya Olimpiki Kenya Nock Paul Tergat.

Categories
Michezo

Kenya Morans wajikaza kisabuni lakini waambulia kichapo dhidi ya Senegal

Timu ya taifa ya Kenya ya mpira wa Kikapu maarufu kama Morans ilijizatiti katika mechi yake ya kwanza ya kundi B Ijumaa adhuhuri kabla ya kusakamwa na vigogo Senegal pointi 51-69 katika mechi iliyopigwa katika ukumbi wa Palais Polyvalent des Sports  mjini Yaounde Cameroon.

Morans walipoteza  robo ya kwanza alama 18-21 kabla ya kuimarika na kunyakua robo ya pili pointi  13-6 ikiwa pia mara ya kwanza kwa Kenya kushinda robo ya mchezo dhidi ya Senegal.

Hata hivyo maji yalizidi unga kwenye robo ya tatu ,Kenya wakiadhibiwa alama 10-25 na kisha wakalazwa  robo ya mwisho 10-17.

Licha ya kupoteza mchuano huo kocha wa Kenya Liz Mils amesema amejivunia mchezo wa Morans ikilinganishwa na mwaka jana nchini Rwanda katika mzunguko wa kwanza wa kufuzu walipocharazwa na Senegal pointi 92-54.

“mimi najivunia mchezo wa timu yangu  haswa katika robo mbili za mchezo huo,na ile ya pili,ukilinganisha na nchini Rwanda mwaka jana tulijituma ,na wakati mwingine  tukikutana na Senegal mambo yatabadilika”akasema Mils

Morans watarejea uwanjani Jumamosi usiku kukabiliana na timu ya pili bora Afrika, Angola,kabla ya kuhitimisha ratiba dhidi ya Msumbiji Jumapili Jioni.

Kenya ni ya tatu katika kundi B kwa pointi 4 baada ya kushindwa na Angola na Senegal na kuishinda Msumbiji katika mkondo wa kwanza wa mechi hizo za kufuzu ulioandaliwa Kigali Rwanda mwaka uliopita.

Timu 16 zitafuzu kushiriki makala ya 30 ya mashindano ya FIBA Afrobasket mjini Kigali  baina ya Agosti24 na Septemba 5  mwaka huu.

Categories
Michezo

Pamzo ateuliwa kocha msaidizi wa Gor Mahia

Sammy ‘Pamzo Omollo’ ameteuliwa kuwa naibu kocha wa mabingwa wa Kenya Gor Mahia .

Omollo, ambaye alikuwa beki wa zamani wa Kogalo anatarajiwa kusafiri na timu hiyo kwa mechi ya marudio kufuzu kwa hatua ya makundi Jumapili dhidi ya NAPSA Stars ya Zambia.

Omollo anatwaa mikoba hiyo ya naibu kocha wa Kogalo  kusaidiana na kocha mkuu  Mreno Carlos Manuel Vaz Pinto na ndiye naibu kocha wa kwanza tangu kuondoka kwa Patrick Odhiambo  aliyehamia Kakamega Homeboyz.

Kocha huyo hajakuwa na kibarua tangu afurushwe Posta Rangers akiwa kocha mkuu kutokana na matokeo mabovu,na ni mara yake ya pili kurejea Gor baada ya kuwa usukani katika mechi za ligi ya mabingwa msimu huu .

Gor Mahia walioshindwa bao 1-0 katika mkumbo wa kwanza wiki jana watawania ushindi wa magoli 2-0 Jumapili ili kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe hilo kwa mara ya pili.

Categories
Michezo

Leopards kukabana koo Rangers wakati Ulinzi wakipambana na Sofapaka Betway Cup

Vigogo AFC Leopards  wameratibiwa kuwaalika  Posta Rangers katika mechi za awamu ya 32 bora kuwania kombe la Bet way kwa mjibu wa droo iliyoandaliwa mapema Ijumaa.

Kwenye ratiba nyingine itakayoshirikisha vilabu kutoka ligi kuu Ulinzi stars watakuwa na miadi dhidi ya Sofapaka huku mechi hizo zikichezwa baina ya April 17 an 18.

Mabingwa wa mwisho wa kombe hilo Bandari fc wamepangwa dhidi ya Dimba Patriots ,Tusker wachuane dhidi Marafiki FC  nayo timu ya kaunti ya Tranz Nzoia Transfoc FC iwe mgeni wa Kenya Commercial Bank.

Timu itakayotwaa kombe hilo itatuzwa shilingi milioni 2 na nafasi ya kuiwakilisha Kenya katika mashindnao ya kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Ratiba kamili ya mechi za raundi ya 32 bora

 1. Fortune Sacco vs Nairobi City Stars
 2. Congo Boys / Gor Mahia vs CUSCO
 3. Marafiki vs Tusker
 4. Sofapaka vs Ulinzi Stars
 5. AFC Leopards vs Posta Rangers
 6. Malindi Progressive vs Luanda Villa
 7. Bandari vs Dimba Patriots
 8. Bungoma Superstars vs Nation FC
 9. KCB vs Transfoc
 10. Kariobangi Sharks vs Tandaza
 11. Kajiado North vs Sigalagala TTI
 12. Equity vs Keroka TTI
 13. Twomoc vs Vegpro
 14. Bidco United vs Twyford
 15. Egerton vs Administration Police
 16. Mara Sugar vs NYSA
Categories
Michezo

Burkina Faso na Tunisia wasajili ushindi AFCON U 20

Timu za Burkina Faso na Tunisia zilisajili ushindi wa kwanza  katika kundi B  katika mashindano ya kuwnaia kombe la Afrika kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20 yanayoendelea nchini Mauritania.

Tunisia walisajili ushindi wa mabao 2-0  dhidi ya Namibia katika mechi ya kwanza uwanjani Cheikh Ould Boidiya   mjini Nouakchott Mauritania na kuweka hai matumaini ya kufuzu hatua ya mwondoano  .

Marc Martin Lamti na Hassan Ayari walipachika mabao yote moja kila kipindi  na kuiweka Tunisia katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali  wakiwa wamezoa pointi 4 kutokan an mechi 2 nao Namibia wananing’inia kubanduliwa wakiwa na alama 1.

Katika mkwangurano mwingine  wa pili kundini B ,Burkina Faso walitoka nyuma na kulazimisha ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati .

Isaac Ngoma aliwaweka Afrika ya kati uongozini kufutia kosa la  dakika ya 32 ,lakini Burkina Faso wakarejea mchezoni kwa goli la dakika ya 2 ya ziada ya Joefrey  Bazie na timu zote kwenda mapumzikoni wakiwa sara ya 1-1.

Eric Chardey aliongeza bao la pili kwa  Burkina Faso dakika ya 52  naye Pindwinde Beleme  akakongomelea msumari wa mwisho kwa jahazi la Afrika ya Kati kwa goli la 3.

Burkina Faso wamezoa pointi 4 baad ya mechi 2  sawa na Tunisia huku Afrika ya kati na Namibia wakiwa na alama 1 kila moja.

Kipute hicho kuendelea Ijumaa jioni kwa mechi za kundi C ,Tanzania waliopoteza mechi ya kwanza wakikabiliana na Gambia saa moja usiku ,kabla ya Ghana kumaliza udhia na Moroko saa nne usiku.

Categories
Michezo

Shujaa na Lioness kujipima makali Madrid 7’s

Timu za taifa za kenya kwa wachezaji 7 kila upande zitashuka uwanjani kwenye  mashindano ya mwaliko ya Madrid 7’s Jumamosi hii ,huku zikitumia mashindano hayo ya wiki moja kujitayarisha kwa michezo ya Olimpiki mjini Tokyo Japan.

Timu ya vipusa maarufu kama ,Lionesses watafungua ratiba dhidi Urusi kabla  ya kupambana na USA na kumenyana na  Ufaransa  .

Jumapili  Lionesses watapambana dhidi ya Uhispania na Poland .

Shujaa watapiga mechi ya kwanza dhidi ya Ufaransa Jumamosi  ,kabla ya kukabiliana na Ureno na  USA na  kurejea uwanjani tarehe 21  dhidi ya wenyeji Uhispania na Argentina .

Timu za Kenya  zilipata fursa ya kumtembelea balozi wa Kenya nchini Uhispania Richard Opembe Alhamisi jioni mjini Madrid.

Bakozi wa Kenya nchini Uhispania Richard Opembe akikutana wachezaji na maafisa wa timu za Kenya

Lionesses Fixtures EAT (GMT+3)
20 February
12.22pm Russia v Lionesses
2.45pm  USA v Lionesses
5.30pm France v Lionesses

21 February
12.22pm Spain v Lionesses
3.29pm Poland v Lionesses

Shujaa Fixtures EAT (GMT+3)
20 February
1.50pm Shujaa v France
4.35pm Shujaa v Portugal
7.20pm Shujaa v USA

21 February
1.28pm Shujaa v Spain
4.13pm Shujaa v Argentina

Wachezaji na maafisa wa kenya wakikutana na balozi wa kenya Uhispania Richard Opembe