Casa Mbungo atua Bandarini kupiga ukufunzi kwa miaka miwili

Andre Cassa Mbungo ameteuliwa  kuwa kocha mpya wa kilabu cha Bandari FC chenye makaoa yake pwani ya Kenya kwa kandarasi ya miaka miwili .

Mnyarwanda huyo  mwenye umri wa miaka 51 na ambaye msimu jana aliifunza  AFC Leopards atasaidiwa  na aliyekuwa kocha msaidizi wa  Gor Mahia Patrick Odhiambo katika majukumu yake mapya.

Kibarua cha kwanza cha Mbungo kitakuwa kuiongoza Bandari dhidi ya washindi mara 11 wa ligi kuu  humu nchini Tusker Fc katika pambano la ligi kuu FKF.

Kocha huyo amesema lengo lake Bandarini ni kunyakua mataji .

 

CEO wa Bandari   Edward Oduor

Mabingwa watetezi wa ligi Gor Mahia pia wamekuwa wakinyemelea huduma za kocha huyo lakini mwenyewe akaamua kutua Bandari

“Ulikuwa uamuzu rahisi kwangu baada ya Bandari kunionyesha kuwa wanahitaji huduma zangu na niwapa kipa umbele badala ya Gor Mahia”akasema Mbungo

Bandari  inashikilia nafasi ya sita ligini kwa alama nane baada ya kucheza mechi sita.

Baada ya kuigura Ingwe mwaka 2019 Mbungo alirejea nyumbani Rwanda na kuifunza  Gasogi United kabla ya kuhamia Rayon Sports .

Mbungo aliigura Ingwe Disemba mwaka 2019 kwa kutolipwa mshahara wake.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *