Cameroon na Mali zawinda nafasi ya robo fainali

Wenyeji Indomitable Lions ya Cameroon na Flying Eagles ya Mali watakuwa wakiwania tiketi ya kwanza kucheza robo fainali ya makala ya 6 ya kombe la CHAN watakapopambana Jumatano usiku katika mchuano wa kwanza wa raundi ya pili uwanjani Ahidjo Amadou  mjini Yaounde Cameroon.

Timu hizo zitakutana katika mechi ya kundi A ikiwa ni mara ya pili katika historia baada ya Cameroon kuwashinda Mali bao 1-0 katika makala ya CHAN mwaka 2011 nchini Sudan.

Mataifa yote yaliafungua makala ya mwaka huu ya CHAN kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe na Burkinafasso Jumamosi iliyopita huku pia ikisadifu magoli yote kufungwa kuanzia dakika za 70  na 72 .

Kocha wa Mali Nahoum Diane’ ambaye ana uzoefu mkubwa atajaribui kutumia vyema safu yake ya ushmabulizi na mabeki ili kupata matokeo huku Indomitable Lions pia wakijivunia safu imara ya nyuma.

Sare pia itafaidi pande zote na kuwafuzisha robo fainali endapo mchuano wa pili kati ya Burkinafasso na Zimbabwe utaishia sare.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *