Cameroon na Mali watoshana nguvu huku Burkina Fasso ikiwatimua Zimbabwe CHAN

Wenyeji Cameroon maarufu kama Indomitable Lions na Flying Eagles ya Mali  zilitoka sare  ya bao 1-1   katika uwanja wa Ahidjo Ahmadou mjini Doula,mchuano  wa kundi A uliochezwa Jumatano usiku .

Cameroon walitangulia kufunga bao katika dakika ya 6  kupitia kwa Salomon Bindjeme 2 kabla ya Issaka Samake kuisawazishia Mali kunako dakika 12 na kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya 1-1.

Timu zote zilicheza kwa tahadhari kuu huku mchuano ukimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Matokeo hayo yanamaanisha kuwa timu zote zina fursa ya kufuzu kwa robo fainali zikiwa na alama 4 kila moja huku wakimaliza mechi zao Jumapili ijayo  ambapo Cameroon watacheza na Burkinafasso huku Mali wakihitimisha ratiba dhidi ya  Zimbabwe.

Katika pambano la pili Jana usiku Zimbabwe inayofunzwa na kocha Zdravko Lugarisic ilikuwa timu ya kwanza kubanduliwa katika mashindano ya mwaka huu baada ya kupoteza mabao 3-1 kwa Burkina Fasso  katika uwanja wa Ahidjo Amadou.

Issouf Sosso alifungua ukurasa wa magoli kwa Burkinafasso katika dakika ya 14 kabla ya Partson Jaure kusawazisha katika dakika ya 23 na kipindi cha kwanza kuishia sare ya 1-1.

Claver Kiendrébéogo aliwarejesha Burkinafasso uongozini kwa bao la pili dakika 53 naye Issiaka Ouédraogo kupachika bao la tatu dakika ya 67.

Cameroon wangali kuongoza kundi hilo kwa pointi 4 sawa na Mali wakifuatwa na Burkina Fasso kwa alama 3 wakati Zimbabwe ikiwa bila alama.

Mechi mbili za kundi B kupigwa Alhamisi Libya wakifungua ratiba dhidi ya Congo DR nao Niger wacheze na Congo Brazaville saa nne usiku.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *