Cameroon kusukumwa na mashabiki wa nyumbani CHAN

Mataifa 16 yako nchini Cameroon kushiriki  mashindano  ya Afrika kwa wachezaji wanaosakata  soka katika ligi za nyumbani maarufu  CHAN  yatang’oa nanga rasmi Jumamosi hii.

Mataifa hayo 16 yametengwa katika makundi manne ya timu 4 kila moja huku mechi hizo 32 zikiandaliwa katika viwanja 4 vilivyo katika miji mitatu  nchini Cameroon .

Tuangazie  Cameroon iliyo  katika kundi A ambalo linajumuishwa wenyeji pia ,Zimbabwe,Mali na Burkinafasso.

Cameroon watacheza pambano la ufunguzi Jumamosi dhidi Zimbabwe  kuanzia saa moja katika kundi A kabla ya kuwapisha Mali watakaomenyana na Burkinafasso saa nne usiku mechi zote zikipigwa katika uwanja wa Limbe.

Cameroon watakuwa wakicheza CHAN kwa mara ya nne wakicheza hadi robo fainali mara mbili mwaka 2011 na 2016 , ingawa walishindwa kutoka kwa kundi lao katika makala ya mwaka 2018 ,  na watakuwa wakiongozwa na Martin Ndtoungou Mpile .

The Indomitable Lions inajivunia wachezaji  beki Banga Bindjeme aliyekuwa CHAN mwaka 2018 na mshambulizi mzoevu Jacques Zoa.

Wenyeji watakuwa na msukumo wa kipekee baada ya serikali na waandalizi wa michuano hiyo kuruhusu mashabiki wa nyumbani pekee kuingia uwanjani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *