Caf yaahirisha nusu fainali za ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho

Shirikisho la soka barani Afrika Caf limeahirisha siku za kuchezwa kwa nusu fainali za ligi ya mabingwa na kombe la shirikisho kutoka Septemba hadi Oktoba mwaka huu.

Nusu fainali ya ligi ya mabingwa ilipaswa kucheza Septemba 22 huku ile ya kombe la shirikisho ikipigwa tarehe 25 mwezi huu.

Kulingana na taarira kutoka kwa Caf ,wamelazimika kuchukua hatua hiyo, kutokana na ombi   kutoka shirikisho la soka nchini Moroko kutaka mechi hizo zisongezwe mbele  kutokana na janga la covid 19 ambalo limesababisha kupigwa marufuku kwa usafariri kutoka na kuingia nchini humo.

Hatua hii ina maana kuwa mikondo ya kwanza ya ligi ya mabingwa itachezwa Oktoba 17 na 18 , huku mechi za marudio zikiandaliwa siku 6 baade nayo fainali ipigwe Novemba 6.

Esperance wakitwaa kombe la ligi ya mabingwa mwaka jana

Raja Casablanca ya Moroko itapambana na  Zamalek ya Misri katika nusu fainali ya kwanza ,nao   Wydad Casablanca wapambane  dhidi ya  Al Ahly  pia ya Misri katika nusu fainali ya pili.

Nusu fainali za kombe la shirikisho ambazo zitachezwa kwa mkondo mmoja pekee zitachezwa Oktoba 19 na 20 wakati fainali ikiratibiwa Oktoba 25.

Pyramids F.C.ya Misri itavaana na AC Horoya ya Guinea katika nusu fainali ya kwanza ,huku  RS Berkane ya Moroko ikimaliza udhia   na Hassania Agadir kutoka Moroko.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *