Burkinafasso wacheza CHAN kwa mara ya 3

Burkinafasso wanafahamika kama the Stallions na watakuwa Cameroon kucheza Michuano ya CHAN kwa mara ya tatu wakicheza mwaka 2014 na 2018 ingawa katika makala yote walishindwa kufuzu kwa hatua ya mwondoano.

The Stallions waliibandua Ghana ili kujikatia tiketi kuelekea Cameroon na wanajivunia mshambulizi matata Yannick Pognongo aliyefunga bao la pekee dhidi ya Black Stars ndiposa wakafuzu.

Wachezaji wengine nyota katika kikosi cha Burkinabe ni Mohamed Lamine Ouattara,beki , Amadou Zon, Hermann Nikièma na  Soumaïla Ouattara na kipa mkongwe Babayouré Sawadogo .

Kocha mkuu wa Burkinafasso ni Seydou Zerbo huku wakipiga mchuano wa ufunguzi  dhidi ya Mali katika kundi A Jumamosi saa nne  usiku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *