Bunge lapendekeza kuanzisha kituo chake cha habari

Bunge linanuia kuanzisha kituo huru cha habari kitakachoangazia  shughuli zake.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuhusu utangazaji na maktaba, Justus Kizito, hatua hiyo inakusudiwa kusaidia wananchi kufuatilia vyema shughuli zinazoendelea katika Mabunge ya Kitaifa na Seneti.

Kizito amesema wabunge watawashirikisha wananchi katika shughuli zao bungeni na kwenye maeneo bunge yao kwa minajili ya uwazi na uwajibikaji.

“Tutaajri waandishi wa habari na vifaa vya kukusanya, kutayarisha na kusambaza habari kutoka kwa wabunge, maeneo bunge na pia kutoka kwa viongozi wengine kama wawakilishi wa akina mama,” akasema.

Kizito amesema hayo wakati wa warsha ya kamati ya bunge kuhusu utangazaji na maktaba jijini Mombasa.

Akiongea kwenye warsha hiyo, Mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji humu nchini KBC, Dkt. Naim Bilal ameahidi kuwa shirika hilo litatoa usaidizi wa kiufundi na ushauri kufanikisha uzinduzi wa kituo hicho.

Dkt. Bilal amesema atashauriana na kamati hiyo katika muda wa majuma mawili yajayo kutafuta mwafaka na kuwasilisha bajeti ya kuanzisha kituo cha utayarishaji vipindi vya bunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *