Bunge kurejelea vikao baada ya likizo ya wiki mbili

Bunge la Kitaifa na lile la Seneti yanatarajiwa kuanza tena vikao vyake Jumanne alasiri, baada ya mapumziko ya wiki mbili.

Wabunge walienda mapumzikoni baada ya kushughulikiwa kwa mswada uliozua utata wa mgao wa mapato ambao ulidumu kwa muda mrefu katika Bunge la Seneti.

Wanaporejea, wabunge wanapaswa kuanza kushughulikia ripoti ya mpango wa maridhiano ya Kitaifa, BBI, kabla ya kura ya maamuzi inayotarajiwa.

Hayo yanajiri wakati Wabunge wa Bunge la Kitaifa na Seneti wakikusanyika huko Naivasha, Kaunti ya Nakuru kujadili ripoti hiyo ya BBI.

Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga pia wanatarajiwa katika mkutano huo ambao unatafuta kukuza msimamo wa pamoja kuhusiana na ripoti hiyo.

Mkutano huo pia unatarajiwa kuratibu mpango wa utekelezaji wa mapendekezo kwenye ripoti hiyo.

Licha ya kuwa kwenye mapumziko, wanachama wa Kamati ya Bunge kuhusu Habari, Mawasiliano na Uvumbuzi walimsaili Immaculate Kassait ambaye aliteuliwa kuhudumu kama Kamishna wa kwanza wa Takwimu.

Rais Kenyatta alimteua Kasait chini ya Sheria ya Ulinzi wa Takwimu ya mwaka 2019.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *