Bunduki milioni 40 zinamilikiwa kinyume cha sheria humu nchini

Takriban bunduki milioni 40 zinamilikiwa kinyume cha sheria hapa nchini hali ambayo inatishia amani na usalama wa kitaifa.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa shirika la  Kenya National Focal Point  kuhusu silaha ndogo ndogo,  Kati ya bunduki hizo milioni 40, kuna bunduki  elfu 64 zinazomilikiwa kinyume cha sheria katika eneo la pwani pekee.

Akiwahutubia wanahabari huko  Hola, mkurugenzi wa shirika la Kenya National Focal Point  Charles Munyoli alisema kuwa licha ya juhudi za kuwahamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kusalimisha silaha hizo, baadhi yao bado wanaendelea kuzimiliki bunduki hizo kinyume cha sheria.

Alisema kuwa machafuko yanayoshuhudiwa katika baadhi ya mataifa jirani, yanatoa mianya ya kuingiza silaha hizo nchini kinyume cha sheria.

Munyoli alisema kuwa umiliki wa bunduki kinyume cha sheria ndio chanzo kikuu cha kuibuka kwa magenge ya uhalifu ya vijana katika eneo la pwani na kusababisha visa vingi vya uhalifu ambavyo vinachangia vifo vya vijana wengi walio na talanta.

Shirika hilo linalenga kukusanya zaidi ya bunduki milioni  15 kufikia mwishoni mwa mwaka huu kupitia kwa mchakato wa kujitolea kwa hiari.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *