Brigid Kosgei na Ruth Jepngetich Kujivinjari mbuga za wanyamapori
Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon Brigid Kosgei na bingwa wa dunia katika mbio za marathon Ruth Jepngetich wametunukiwa fursa ya kutalii mbuga za wanayama pori za Laikipia,Samburu na Lamu kwa muda wa siku tano na halmashauri ya utalii nchini KTB.
Jepngetich na Kosgei wametunukiwa na KTB kwa kuitangaza Kenya kupitia mbio za London marathon mwaka huu ambapo Kosgei aliibuka mshindi huku Jepngetich akimaliza wa tatu.

Afisa mkuu mtendaji wa KTB Dr Betty Radier amewapongeza wanariadha hao kwa jukumu lao muhimu kuitangaza Kenya kupitia riadha na kuahidi kuwa wataendelea kushirikiana na wanariadha kuitangaza Kenya kote ulimwenguni.
“Licha ya mwaka huu kuwa mgumu kutokana na Janga la Covid 19 ,tunashukuru kuwa mbio za London marathon ziliandaliwa huku Brigid na Ruth wakiitangaza Kenya vyema kote ulimwenguni.Tunaamini kuwa ni wakati mwafaka wa kuwashirkihsa wanariadha wetu kuitangaza Kenya kimataifa kama eneo la kitalii”akasem Radier
Wanariadha hao wawili ni wa hivi punde kujiunga na halmashauri ya KTB baada ya Eliud Kipchoge ambaye aliteuliwa kuwa brand ambassador mwaka uliopita baada ya kushinda mbio za London marathon mara 4.
Kosgei na Jepngetich walifurahia hatua hiyo ya KTB huku wakiwa tayari kuzuru mbuga hizo za Wanyama kujifurahisha.