Bouchra Hajij achaguliwa Rais mpya wa shirikisho la voliboli Afrika

Bouchra HAJIJ alichaguliwa Jumapili jioni kuwa rais mpya wa shirikish la Voliboli barani Afrika Cavb , baada ya kupata kura 42 dhidi ya mpinzani wake Dr Amr Elwani wa Misri aliyezoa kura 12.

Kura hizo zilipigwa Jumapili usiku kupitia kikao cha video.

Hajij ndiye rais wa shirikisho la Voliboli nchini Moroko na hadi kuchaguliwa kwake amekuwa makamu wa raisa wa  Cavb ,kabla ya kuteuliwa katika baraza kuu la shirikisho la Voliboli ulimwenguni ambako amekuwa akihudumu kama makamu wa Rais wa FIVB.

Hajij, atahudumu kwa kipindi cha miaka minne hadi mwaka  2024 .

Rais wa shirikiho la Voliboli Kenya Waithaka Kioni alichaguliwa kuwa makamu wa rais wa zone 5 katika uchaguzi huo

Wanabodi wengine waliochaguliwa katika nyadhfa za makamu wa Rais kuwakilisha kila ukanda ni Adnan Bakbak wa Libya kutoka Zone 1,Rodrigues   ANTONIO CARLOS Cape Verde kutoka Zone 2,Casimir   SAWADOGO wa Burkinafasso Burkina Faso akiwa makamu wa rais wa zone 3,Dokony Adiker IDRISS kutoka Zone 4 na

Fredreck   NDLOVU kutoka Zimbabwe akiwakilisha Zone 6.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *