Categories
Burudani

Bobby Shmurda kuachiliwa huru leo

Mwanamuziki Bobby Shmurda wa Marekani amekuwa kizuizini tangu mwaka 2014 kutokana na makosa ya kula njama ya kuua, kumiliki silaha kinyume cha sheria na kuhatarisha maisha.

Kesi yake iliamuliwa mwaka 2016 na akahukumiwa miaka saba gerezani ingawaje hukumu hiyo ilipunguzwa hadi miaka mitano kwa kuzingatia kwamba alikuwa amekaa kizuizini kwa miaka miwili akisubiri hukumu.

Mwanzo wa mwaka huu, kamati ya kushughulikia muda wa vifungo iliamua kumpa Shmurda tarehe 23 mwezi Februari mwaka huu wa 2021 kama siku ya kuachiliwa huru.

Mamake mwanamuziki huyo alisema kwamba ana matumaini makubwa anapotizamia kumlaki mwanawe nyumbani baada ya muda mrefu na kwamba Bobby ameamua kutulia kwa sasa.

Mzazi huyo alifichua pia kwamba mwanawe anataka kurejelea kazi ya muziki mara moja.

Bobby Shmurda hata hivyo atakuwa chini ya uangalizi wa idara hiyo ya kurekebisha tabia kwa muda wa miaka mitano ijayo ndipo awe huru kabisa.

Kifungo chake kingekamilika mwisho wa mwaka huu wa 2021 lakini wasimamizi waliamua kumpunguzia kutokana na tabia yake nzuri akiwa kwenye jela na jinsi amekuwa akijihusisha na mipango tofauti yenye lengo la kurekebisha tabia.

Mwanamuziki mwenzake kwa jina Quavo ameahidi kwenda kumchukua Bobby kutoka kwenye jela iitwayo “Clinton Correctional” huko New York kwa njia ya kipekee.

Quavo

Ackquille Jean Pollard au ukipenda Bobby Shmurda alizaliwa mwaka 1994 na akaingilia muziki mwaka 2014. Alisajiliwa na kampuni ya muziki kwa jina “Epic Records” mwaka huo wa 2014 baada ya wimbo wake “Hot nigga” kuwa namba 6 kwenye Billboard.

Mkusanyiko wa nyimbo zake za kwanza ambazo alizipa jina “shmurda She Wrote” ulizinduliwa mwezi Novemba mwaka 2014 naye akakamatwa mwezi Disemba mwaka huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *