Bingwa wa dunia Timothy Cheruiyot kuwika Kip Keino Classic Jumamosi

Bingwa wa dunia katika mbio za mita 1500 Timothy Cheruiyot atalenga kufunga msimu kwa njia ya kipekee na  jumamosi hii atakapotimka mbio hizo kwenye mashindano ya Kip Keino Classic katika uwanja wa taifa wa Nyayo.

Cheruiyot ameanza mwaka huu vyema kwa kuandikisha muda kasi katika mashindano ya diamond league  mjini Monaco Ufaransa kwa kusajili dakika 3 sekunde  28 nukta 45 mwezi Agosti.

Baadae alishinda mkondo wa Stockhom nchini Uswidi katika mashindano ya Diamond league Agosti 23.

Cheruiyot akiwa na kocha wake Bernard Ouma

Cheruiyot ambaye pia ni mshindi wa diamond league msimu jana anasema lengo lake leo ni kushinda nap engine kusajili muda wa kasi ili kuwatumbuiza  mashabiki.

Kocha wake Bernard Ouma pia ana Imani kwamba Cheruiyot amejiandaa vyema huku akiongeza kuwa mashidndano ya leo yatawapa fursa wanariadha wa humu nchini kutamba mbele ya mashabiki wa Nyumbani .

Cheruiyot anasema janga la ugonjwa wa Covid 19 limesitisha mipango yake huku akilenga dhahabu ya Olimpiki mwaka ujao kauli ambayo ni sawa na ya mkufunzi wake.

kwa jumla kutakuwa na wanariadha watatu kutoka kambi ya Rongai Athletics Club wanaofunzwa na Kocha Ouma katika mashindano ya Jumamosi jioni.

Katika fainali ya mita 1500 jumamosi hii Cheruiyot atapambana na Silas Kipalgat,Abraham Rotich,Abel Kipsang,Kumari Taki,Timothy Sein,Vincent Keter ,Bethwell Birgen ,Barjir Hiss wa Djibouti,Weinans Valentijn wa Uholanzi  na Abdoufatah Daher wa Djibouti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *