Bingwa wa dunia Cheptegei kupandishwa cheo katika idara ya polisi Uganda

Inspekta mkuu wa polisi nchini Uganda John Martins Okoth Ochola amependekeza kupandishwa cheo kwa bingwa wa dunia wa mbio za mita 10,000  Joshua Cheptegei katika kikosi cha polisi wa Uaganda Police Force.

Akiwatubia wanahabari mapema Jumatatu msemaji wa polisi , Fred Enanga alisema kuwa kamati ya ushauri ikiongozwa na  Ochola  iliketi wiki iliyopita na kupitisha hoja ya kupandishwa madaraka kwa polisi huyo ambaye anashikilia rekodi za dunia za mita 10,000 na mita 5,000.

Cheptegei atapandishwa cheo kutokana na matokeo mazuri aliyosajili katika mashindano ya kimataifa na kwa mjibu wa pendekezo hilo atapandishwa cheo hadi wahfa wa Assistant Superintendent of Police cheo chenye mawe matatu.

Mwanariadha huyo aliye na umri wa miaka 24 ambaye hushiriki mbio za masafa marefu alivunja rekodi ya dunia maajuzi ya mita 10,000 aliposajili dakika 26 sekudne 11 katika mbio za Valencia akifuta rekodi ya Kenenisa Bekele wa Ethiopia  kwa Zaidi ya sekunde 6.

Awali pia Cheptegei alivunja rekodi ya dunia ya mita 5,000 Agosti 14 katika mashindano ya Diamond league mjini Monaco Ufaransa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *