Binadamu waambukizwa homa ya ndege aina ya H5N8 Russia

Russia imeripoti kisa cha kwanza cha homa ya ndege wa kufugwa aina ya H5N8 inayoambukiza binadamu.

Maafisa wa serikali wamesema wahudumu saba kwenye kiwanda kimoja cha ndege wa kufugwa kusini mwa nchi hiyo wameambukizwa homa hiyo iliyozuka mwezi wa Disemba.

Afisa mkuu wa halmashauri ya afya nchini humo Anna Popova alisema hatua za haraka zimechukuliwa kuzuia kuenea kwa homa hiyo.

Alisema kisa hicho kimeripotiwa kwa shirika la afya duniani-WHO.

“Habari kusuhu maambukizi ya homa hiyo ya ndege kwa binadamu, tayari imewasilishwa kwa shirika la Afya la umoja wa mataifa,” alisema Popova.

Aina nyingine ya homa za ndege iliyo na uwezo wa kuambukiza binadamu imesababisha vifo,lakini hii ni mara ya kwanza ya homa hiyo ya H5N8 kuambukiza binadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *