Biden amushtumu Trump kwa kuchelewesha mswaada wa malipo kwa waathiriwa wa janga la COVID-19 Marekani

Rais mteule wa Marekani Joe Biden ameonya kwamba kutakuwa na matokeo mabaya zaidi ikiwa Rais Donald Trump ataendelea kuchelewa kutia saini mswaada wa sheria ya kuwanusuru raia wa taifa hilo kutokana na matatizo yaliyosabaishwa na janga la ugonjwa wa COVID-19.

Amesema mpango wa marupu rupu kwa wasio na ajira na pia marufuku dhidi ya visa vya kuwafurusha watu utaathiriwa ikiwa mswaada huo hauatiwa saini kufikia Jumamosi.

Mpango huo wa fidia ya dola bilioni 900 uliidhinishwa na Bunge la Congress baada ya majadiliano magumu na kulegezwa kwa misimamo.

Mswaada huo unajumuisha malipo ya dola 600 kwa raia wenye pato la chini ya dola elfu 75 kwa mwaka.

Aidha, Trump anasema angependa watu wasio na ajira nchini humo kupewa marupu rupu ya dola 2,000, lakini wajumbe wa chama cha Republican kwenye Bunge la Congress wamekataa marekebisho hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *