Biden ampiku Trump kwenye matokeo ya mapema ya Urais nchini Marekani

Mgombea Urais wa Marekani wa chama cha Democratic Joe Biden anaongoza kwa kura 223 za majimbo muhimu ya taifa hilo.

Naye Rais Donad Trump amejipatia kura 173, kwenye uchaguzi wa urais ambao umeibua msisimko mkubwa.

Biden alianza kwa ushindi mkubwa katika majimbo muhimu, huku wote wawili wakipania kupata kura 270 za majimbo muhimu ili kuibuka na ushindi.

Wakati uo huo shirika la upelelezi nchini humo FBI linachunguza madai kwamba baadhi ya wapiga kura walipigiwa kura na roboti wasijitokeze kupiga kura.

Kulingana na shirika la habari la AP shughuli ya kuhesabu na kujumuisha kura iliendelea bila matatizo yoyote.

Trumpm mwenye umri wa miaka 74 anajaribu kuepusha kushindwa kwenye uchaguzi huu wa urais na kuwa rais wa kwanza kuongoza kwa kipindi kimoja tangu Rais George Bush mwaka wa 1992.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *