Biden amkashifu Trump kwa jinsi anavyoshughulikia janga la Korona Marekani

Mwaniaji Urais wa chama cha Democratic nchini Marekani Joe Biden amekosoa jinsi Rais Donald Trump anavyoshughulikia janga la COVID-19 nchini humo.

Biden amesema hayo alipokuwa akijipigia debe kwa wapigaji kura wazee katika jimbo muhimu la kiuchaguzi la Florida.

Biden amewaambia kwamba rais huwa hawatilii maanani wazee ambao wanakabiliwa na hatari zaidi kutokana na janga hilo.

Kuna tofauti kubwa ya sera baina ya wawaniaji hao wawili kuhusiana na janga la COVID-19.

Na huko Pennsylvania, Trump amewaambia maelfu ya wafuasi wake kwamba anajihisi buheri wa afya baada ya kutibiwa na kupona kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Rais Trump alithibishwa kuwa na virusi hivyo tarehe mosi mwezi huu na kukaa hospitalini kwa siku tatu kabla kuruhusiwa kuondoka mwishoni mwa juma lililopita.

Trump alirejelea kampeni zake mara moja kwa kuandaa mkutano huko Florida.

Wawili hao wanatarajiwa kukabana koo kwenye uchaguzi wa Urais nchini humo ulioratibiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *