Bendera ya Kenya kupeperushwa New York

Bendera ya Kenya leo usiku itapeperushwa nje ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Kulingana na Wizara ya Mashauri ya Kigeni, hafla ya kutangazwa rasmi kwa wanachama wapya wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa itafanyika mwendo wa saa mbili leo usiku.

Kenya itakuwa mwanachama wa baraza hilo kwa kipindi cha miaka miwili.

Kenya inachukua mahala pa Afrika Kusini baada ya kuishinda Djibouti kwenye kura.

Kenya sasa inajiunga na Tunisia na Niger ambazo pia zinawakilisha Bara la Afrika kwenye baraza hilo la usalama.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lina wanachama kumi wasio wa kudumu na watano wa kudumu ikiwemo Marekani, Ufaransa, Uingereza, China na Urusi.

Baadhi ya majukumu ya baraza hilo ni kudumisha amani na usalama duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *