Categories
Habari

Bei ya Petroli yaongezeka huku ya mafuta taa ikisalia kama ilivyo

Bei ya lita moja ya mafuta aina ya petroli inatarajiwa kuongezeka kwa senti 72 kuanzia saa sita usiku tarehe 15 Oktoba, 2020, kufuatia mabadiliko ya kila mwezi ya halmashauri ya kudhibiti kawi na mafuta.

Aidha, lita moja ya mafuta ya diseli imepungua kwa shilingi mbili na senti 18 huku bei ya mafuta taa ikisalia jinsi ilivyo.

Takwimu za halmashauri ya kudhibiti kawi na mafuta zinaonyesha kwamba gharama ya uagizaji ‘super petrol’ iliongezeka kwa asilimia 1.12 huku ile ya ‘diesel’ ikishuka ikwa asilimia 5.4.2.

Bei ya mafuta taa haijabadilika kwani hakuna shehena ambayo imeruhusiwa kuondoka katika bandari ya Mombasa.

Kawi itauzwa kwa bei ya chini zaidi mjini Mombasa ambako lita moja ya super petrol itagharimu shilingi 104 na senti 86 huku dizeli ikiuzwa kwa shilingi 90 na senti 53, nayo mafuta taa yatauzwa kwa shilingi 81 na senti 37.

Jijini Nairobi, lita moja ya petroli aina ya Super itaongezeka hadi shilingi 107 na senti 27, dizeli itashuka hadi shilingi 92 na senti 91 huku mafuta taa yakiuzwa kwa shilingi 83 na senti 73.

Mafuta yatakuwa ghali zaidi huko Mandera ambako lita moja ya super petrol itauzwa kwa shilingi 120 na senti 30, dizeli itauzwa kwa shilingi 105 na senti 96 nayo mafuta taa yatagharimu shilingi 96 na senti 77.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *