Bei ya mafuta yaongezwa hapa nchini

Gharama ya nauli pamoja na bei ya bidhaa muhimu huenda ikaongezeka baada ya halmashauri ya kudhibiti sekta za kawi na mafuta nchini-EPRA, kuongeza bei ya mafuta nchini.

Kulingana na halmashauri hiyo, kuanzia Alhamisi usiku wa manane, wakenya watalazimika kuongeza shilingi  3 na senti 56 ili kununua lita moja ya mafuta taa.

Bei ya petroli ya Super iliongezeka kwa senti 17. Sasa lita moja ya petrol ya super itauzwa kwa shilingi 106 na senti 99 jijini Nairobi.

Mafuta ya  diesel yatauzwa shilingi 96 na senti 40 kwa lita huku mafuta taa yakiuzwa kwa shilingi 87 na senti 12 kwa lita.

Mafuta yatakuwa ghali Mandera ambapo lita moja ya petrol ya  super itakuwa ikiuzwa kwa shilingi  120 na senti 3.

Mafuta ya diesel yatakuwa yakiuzwa kwa shilingi 109 na senti 44 kwa lita huku mafuta taa yakiuzwa kwa shilingi mia moja na senti 17.

Mabadiliko hayo ya bei yanatokana na kuongezeka kwa gharama za bidhaa hizo katika soko la kimataifa katika miezi kadhaa iliyopita na pia kufifi kwa shilingi ya kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *