Categories
Habari

BBI yapita magatuzini, sasa yaelekea Bunge la Kitaifa

Mswada wa marekebisho ya katiba ya mwaka 2020 kupitia mpango wa maridhiano ya kitaifa (BBI) umetimiza uungwaji mkono wa mabunge 24 yanayohitajika kikatiba ili uelekezwe katika Bunge la Kitaifa kujadiliwa.

Hii ni baada ya mabunge ya Kaunti 12 zaidi kupitisha mswada huo siku ya Jumanne na hivyo kutimiza matakwa ya kikatiba ya kupitishwa na angalau mabunge ya kaunti 24 ambayo ni zaidi ya nusu ya mabunge yote ya kaunti 47 nchini.

Kufikia Jumatatu alasiri, mabunge 12 yalikuwa tayari yamepitisha mswada huo, yakiwemo Homabay, Siaya, Kisumu, Pokot Magharibi, Busia, Trans Nzoia, Kajiado, Kisii, Vihiga, Nairobi, Laikipia na Samburu, huku kaunti ya Baringo ikiwa ya pekee iliyokataa mswada huo.

Mabunge mengi ya kaunti yalikuwa yameratibu kujadili mswada huo Jumanne huku yale ya Kakamega, Narok, Makueni, Nyamira, Taita Taveta, Murang’a, Bungoma, Kitui, Nyeri, Lamu, Nyandarua na hivi sasa Garissa pia limepitisha mswada huo na kutimiza idadi ya 24.

Haya yanajiri huku kaunti zengine zikiendelea kujadili msawa huo na zengine zikiwa bado zinachukua maoni ya wananchi.

One reply on “BBI yapita magatuzini, sasa yaelekea Bunge la Kitaifa”

Well presented…BBI has been passed by county assemblies na hii in kutokana na kipengele cha kuongeza ugavi wa fedha katika county

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *