Balozi wa Iran atoa wito wa ushirikiano ili kukabiliana na silaha haramu Afrika

Balozi wa Iran humu nchini Dkt. Jafar Barmaki amehimiza haja ya ushirikiano baina ya mataifa ya Bara la Afrika ili kukabiliana na changamoto zinazokumba mataifa hayo ikiwemo mizozo ya ndani kwa ndani.

Barmaki amesema licha ya juhudi zinazofanywa kukabiliana na changamoto zengine zinazoathiri bara hili, mizozo na ugaidi zimebakia kuwa changamoto kuu katika maeneo kadhaa ya Afrika.

Amesema hali hii imeulazimu Muungano wa Mataifa ya Afrika (AU) ambao unashirikiana na mataifa wanachama kuongoza mpango wa kukabiliana na silaha haramu barani humu.

Balozi huyo amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Hafla ya Kimataifa ya Katuni, inayohusu matumizi ya Sanaa na tamaduni katika juhudi za kuzima silaha Afrika, mashindano yanayohusisha wasanii mbali mbali wa katuni kote ulimwenguni.

Mashindano hayo yataendelea kuanzia Desemba 2020 hadi Mei 2021.

Barmaki amesema mpango huo uliathiriwa vibaya na janga la virusi vya Corona lakini akasisitiza haja ya kuchanganya kauli za 2020 na 2021 ili kuafikia malengo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *