Baba Mtakatifu ataja itikadi kali kuwa ‘usaliti wa dini’

Baba mtakatifu Francis amelaani kile ametaja kuwa itikadi kali kwa kisingizio cha dini katika ziara yake ya kihistoria nchini Iraq ambapo alizungumzia shida za Wakristo walio wachache nchini humo.

Iraq imegubikwa na vurugu za kidini, sio tu dhidi ya wachache lakini pia kati ya makundi ya Waislamu wa Shia na Sunni.

Akiwa nchini Iraq,Baba mtakatifu pia alitembelea mmoja wa viongozi wa waislamu wa Shia mwenye ushawishi mkubwa.

Akihutubia mkutano wa viongozi mbali mbali wa kidini, alikashifu ghasia ambazo zimeghubika Iraq katika muda wa miaka kadhaa huku akitoa wito wa urafiki na ushirikiano miongoni mwa dini mbali mbali.

Jamii zote za kikabila na kidini zimeteseka. Haswa ningependa kutaja jamii ya Yazidi ambayo imeomboleza vifo vya wanaume wake na kushuhudia maelfu ya wanawake, wasichana na watoto wakitekwa nyara, kuuzwa kama watumwa na kupigwa,” alisema kiongozi huyo wa kanisa katoliki.

Akipokea kiongozi huyo wa dini ya katoliki duniani nyumbani kwake katika mji wa Najaf, Ayatollah Ali al-Sistani alisema Wakristo pia wanapaswa kuishi kwa amani na usalama sawa na raia wengine wa Iraq.

Mkutano huo ulikuwa na umuhimu mkubwa ikizingatiwa kwamba hiyo ndiyo ziara ya yake ya kwanza ya kimataifa tangu kuzuka kwa janga la korona ,mwaka moja uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *