B. Simone ajipata pabaya mitandaoni

Muigizaji na mchekeshaji wa Marekani B.Simone ameingiliwa sana na wengi kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram kutokana na maoni yake kuhusu viwango ambavyo wanawake huweka wanapotafuta waume wa kuwaoa.

Kwenye video aliyoipachika kwenye akaunti yake ya Instagram, Simone anahimiza wanawake wawe kile ambacho wanatafuta kwa mwanamume. Kulingana naye ikiwa mwanamke anahiitaji mwanaume ambaye ameajiriwa naye pia lazima aajiriwe.

Akitaka ambaye ana hela naye pia lazima ajifunze kuwekeza pesa zake na ikiwa anataka ambaye ana meno mazuri naye pia lazima ajibidiishe kwa upande huo.

Simone ambaye ana wafuasi zaidi ya milioni tano kwenye Instagram, huwa anatoa maoni yake, vidokezo kuhusu mambo mbali mbali na hata kuchekesha.

Mchekeshaji huyo anamalizia kuhimiza kina dada wajiunge na changamoto aliyoipa jina la “#manifestLoveChallenge” ambapo mwanadada anahitajika kuandika sifa zote ambazo anataka kwa mwanaume na kando ya kila sifa aandike ikiwa ana hiyo sifa yeye mwenyewe.

Hata hivyo watumizi wa mitandao walimrukia Simone kwa maoni hayo yake na kuchagua kumuingilia kutokana na matendo yake ya awali na sauti anayoitumia kwenye video yake.

Wengi walimkumbusha kuhusu makosa aliyosemekana kutenda awali ya kuiba maneno fulani kutoka kwa wengine na kuyatumia kwenye kitabu chake lakini aliomba msamaha mwaka jana akisema hakukusudia kufanya hivyo.

Mwanamuziki Tyrese Gibson hata hivyo alimtetea Simone huku akiahidi kumwajiri hivi karibuni. Gibson aliansika, “Women are pissed? calling her a fraud? But why???? Dear @thebsimone I’m going to hire you as soon as I can.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *