Atletico Madrid yataka kumsajili mshambulizi Luis Suarez

Atletico Madrid imeelezea nia ya kutaka kumsajili mshambulizi Luis Suarez, huku vigogo hao wa Uhispania wakinuia kuipiku Juventus katika usajili wa mchezaji huyo.

Mshambulizi huyo wa Barcelona alihusishwa na kuhamia Turin msimu huu lakini sasa huenda akapata fursa ya kusalia nchini Uhispania. Wakati uo huo, Barcelona inanuia kumruhusu mchezaji Nelson Semedo kuondoka.

Barcelona imehusishwa na usajili wa Hector Bellerin, lakini ni lazima mchezaji mmoja aruhusiwe kuondoka ili kukamilisha usajili huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *