Aston Villa wadumisha rekodi ya asilimia 100% EPL

Timu ya Aston villa ilidhihirisha umahiri wake na kuwa timu pekee iliyoshinda mechi zake zote katika ligi kuu Uingereza ilipokosa adabu za mgeni na kuwaadhibu Leicester City bao 1-0 ugani Villa Park Jumapili usiku.

Leicester walitawala mechi hiyo kwa mashambulizi mengi lakini wakakosa kutumia vyema fursa zao na huku wakitarajia sare waligutushwa na bao la kiungo anayechezea Villa kwa mkopo Rose Barkley katika dakika ya 91 akiunganisha pasi ya kiungo wa Scotland MccGinn.

Villa waliosakata mechi 4 wanakalia nafasi ya pili ligini kwa pointi 12 wakiwa wamefunga mabao 12 na kufungwa mawili.

Everton ni ya kwanza ligini kwa alama 13 kufuatia mechi 5 walizocheza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *