Categories
Burudani

“Asante sana Rais Uhuru Kenyatta”, Diamond Platnumz

Mwanamuziki wa nchi ya Tanzania Diamond Platnumz ambaye pia hujiita Simba au ukipenda Chibu Dangote ni mwingi wa furaha baada ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuchezea kibao chake cha hivi punde zaidi kwa jina “Waah” ambacho alimshirikisha Koffi Olomide.

Diamond aliweka video fupi inayomwonyesha Rais Uhuru Kenyatta na katibu mwandamizi wa maswala ya vijana na uvumbuzi Bi. Nadia Ahmed wakiongozwa kuuchezea wimbo huo kisha akaandika, “Asante sana Rais Uhuru Kenyatta na Kenya nzima kwa upendo. Inaridhisha sana Kuona viongozi wetu wakiunga mkono kazi yetu, sio tu kama wanamuziki lakini vijana wa Afrika.”

Haya yanajiri siku chache tu baada ya mwanamuziki Octopizzo kukashifu wakenya kwa kile ambacho anasema kwamba ni kuwa wanafiki kwa kuunga mkono kazi ya Diamond Platnumz wa Tanzania huku walimtelekeza Otile Brown.

Mwanamuziki huyo ambaye anajulikana kama “Namba nane’s finest” alijibiwa na mashabiki na wafuasi kwenye Twitter ambao walisema wanaunga mkono muziki mzuri na sio jina tu.

Kibao cha Diamond na Koffi kilitazamwa zaidi ya mara milioni mbili kwa muda wa saa kumi na tatu tuu. Diamond anatambua kwamba ana mashabiki wengi nchini Kenya lakini imekuwa muda tangu aandae tamasha humu nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *